Wednesday 3 January 2018

Wapandishwa kizimbani kwa rushwa

Na Gurian Adolf
Nkasi
WATUMISHI Wanne wa halmashauri ya wilaya Nkasi wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa.
Wakisomewa shitaka na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Simeona Mapunda mbele ya hakimu mkazi Rosaria Mgisa washitakiwa hao inadaiwa kuwa Desemba 29  mwaka jana waliomba  na kupokea rushwa ya shilingi milioni 1.2 kutoka kwa mfugaji mmoja mkazi wa kitongoji cha Mumbasi ambaye walikamata mifugo yake ipatayo 40 ndani ya hifadhi ya msitu Wa Mfili ili wasimfikishe kwenye vyombo vya sheria.
Alisema watuhumiwa hao wanashitakiwa chini ya kifungu namba 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Nicodemo Hillu afisa ardhi, na askari wanyamapori ambao ni selivesta Soneka,Justin Makandi,na Anselmo Godian.
Watuhumiwa wote Wanne wameachiwa kwa dhamana na kesi yao itatajwa tena januari 18 mwaka huu.
Akizungumza nje ya mahakama kamanda wa TAKUKURU wilayani Nkasi Samson Bishati alisema kuwa taasisi hiyo imeamua kuwapeleka mahakamani watuhumiwa hao baada ya kukusanya ushahidi wa kutosha.
Mwisho

No comments:

Post a Comment