Katavi
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini mkoani Katavi Sebastian Kapufi ametoa msaada wa baiskeli mbili za kutembele watu wenye ulemavu ambao hawana uwezo wa kutembea kwa miguu.
Msaada huo ameutoa ili kukamilisha ahadi aliyoitoa wakati wa ziara aliyoifanya jimboni kwake kwenye katika Kata za Kawajense na Kasokola ambapo walemavu wawili walimuomba Mbunge huyo awampe msaada wa Baiskeli za kutembele na aliwahidi kuwapatia.
Wakati wa ziara hiyo mbunge huyo alifanya mikutano ya hadhara kwenye Kata hizo na ndipo alipo ombwa baiskeli hizo.
Akizungumza baada ya kubadhiwa baiskeli hiyo Justine Petro (31) mkazi wa mtaa wa Kwajense mwenye ulemavu wa miguu alisema kuwa anamshukuru mbunge huyo kwa kuteleleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mwezi agosti mwaka jana.
Alisema baiskeli hiyo itamsaidia kwani alikuwa hawezi kwenda sehemu yoyote ile bila msaada wa kupelekwa na mtu jambo ambalo kuna wakati lilikuwa kwake linakuwa nigumu na hasa anapokoseka mtu wa kumbeba na kumpeleka anako taka kwenda.
Petro alisema kuwa kuna wakati alikuwa akishindwa hata kwenda kanisani kutokana na wazazi wake kutoku na fedha za kumlipia boda boda hali iliyozidi kumfanya ajione mpwe.
Mbunge wa Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi alisema Baiskeli hizo mbili alizotoa kwa walemavu hao zimegharimu kiasi cha sgilingi 900,000 na ametekeleza ahadi aliyokuwa ameitoa wakati wa ziara yake aliofanya katika kata za Kawajense na Kasokola .
Alisema yeye kama Mbunge wa Jimbo ataendelea kutoa misaada kwenye jamii na wala hata sita kutoa misaada kwa watu wenye mahitaji maalumu kama alivyofanya kwa watu hao wawili.
Bibi Anna John (58) ambaye naye ni mremavu wakutotembea alimshukuru mbunge huyo kwa kutoa msaada huo wa baiskeli kwa Justine John (18) nambaye ni mjukuu wake kwani atawapunguzia gharama za kukodi boda boda mara kwa mara.
Mwisho
No comments:
Post a Comment