Thursday 14 December 2017

Serikali yazuia uvuvi kudhibiti kipindupindu

Na Gurian Adolf
Sumbawanga

SERIKALI mkoani  Rukwa imeagiza kulifunga ziwa Rukwa kwamuda usio julikana kutokana na shughuli za uvuvi kuchungia kasi ya ugonjwa wa kipindupindu katika ziwa hilo.

Mkuu wamkoa huo Joachim Wangabo alitoa agizo hilo wakati akizingumza na wavuvi kwa lengo lakuwaeleza sababu za kulifunga ziwa hilo na kuzuia kabisa uvuvi kutoendelea.

Alisema kuwa baada ya kukaa na wataalamu wa afya wamekubaliana kusitisha shughuli za uvuvi kwani zimekuwa chanzo kikubwa cha kuenea ugonjwa huo. 

"tumekubaliana na wataalamu wa afya  kuwa tusitishe shughuli za uvuvi katika ziwa Rukwa hadi hapo watakapojiridhisha kuwa hakuna ugonjwa wa kipindupindu katika kambi za uvuvi zinazozunguka ziwa hilo vinginevyo itakuwa vigumu kukabiliana na ugonjwa huo hatari"alisema

Alisema kuwa athari inayopatikana katika kambi hizo za uvuvi zitawaathiri wala samaki wanaotokana ziwa hilo hasa waliopo Sumbawanga mjini kwani wanategemea samaki hapo Kama kutoweo na kuwataka walio waliopiga kambi katika ziwa hilo kwaajili ya uvuvi waondoke mara moja kwani hawata ruhusiwa kuingia ziwani kuendelea kuvua samaki. 
Aidha aliagiza kufunguliwa maeneo maalumu kwaajili ya kuwatibia wagonjwa  watakao patikana kwani wasipofanya hivyo mlipuko wa ugonjwa huo utaendelea kuongezeka na watu wengi zaidi wataendelea kupoteza maisha kwa ugonjwa huo. 
Mkuu huyo wa mkoa alifanya  ziara  katika kambi ya wavuvi ya mererani iliyopo katika kijiji cha Ilanga, Kata ya Muze Wilaya ya Sumbawanga katika bonde la Ziwa Rukwa ambapo mpaka sasa Jumla ya wagonjwa 9 waliripotiwa kuugua kipindupindu.
Awali akitoa taarifa ya ugonjwa huo Afisa afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Plasidus Malapwa alisema kuwa ugonjwa huo ulibainika tangu novemba 23 kutokana na mgonjwa aliyetoka kambi ya Lichili, Kijiji cha Lichili, wilayani Momba, Mkoani Songwe na kufia katika kambi ya kamchanga, Kata ya Muze, wilayani Sumbawanga na kuanzia hapo wagonjwa walianza kuongezeka hali iliyosababisha kuanzishwa kwa kambi nne kuzunguka ziwa Rukwa.
“hali ya Wagonjwa hadi kufikia desemba 1 nikuwa katika vijiji vya Muze wagonjwa 6 lakini hakuna kifo, Kipa wagonjwa 8, vifo 2, Kamchanga wagonjwa 26, vifo 3, Matete wagonjwa 6, hakuna kifo hivyo jumla ya wagonjwa wote tangua kuanza kwa mwezi huu ni waginjwa 46 na vifo 5,” alisema
Naye Mganga mfawidhi wa Zahanati ya Muze Dkt Aron Mtolo alisema kuwa, hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kudhibiti ugonjwa huo ikiwamo ni pamoja na kufunga migahawa michafu 8 kuvifungia vilabu vya kuuzia pombe ambapo pia mapipa manne na debe tatu ya pombe  ilimwagwa, na wanywaji pombe 14 walilipishwa faini ya shilingi 20,000 kila mmoja.
Mwisho

No comments:

Post a Comment