Monday, 4 December 2017

RC awaomba viongozi wa dini kuiombea serikali

Na Gurian Adolf
Sumbawanga

MKUU wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaomba viongozi wa dini mkoani humo kuendelea kumuombea rais John Magufuli pamoja na watendaji wengine  wa serikali ili aweze kuwaongoza wananchi kwa kuzingatia misingi ya haki usawa na kuwaletea maendeleo  endelevu.
aliyasema hayo wakati akichangia shilingi milioni moja kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa lengo la kusaidia ujenzi wa kituo cha afya cha Waislamu kinachoendelea kujengwa katika Tarafa ya Kirando, Kata ya Kirando Wilayani Nkasi mkoani humo.
Alisema kuwa rais na watendaji wa serikali ya awamu ya tano wanaitaji kuombewa daima kwani kufanya kazi ya kuwaongoza wananchi sio lelemama hivyo unahitajika msaada wa Mwenyezi Mungu.
Wangabo alisema katika kuwaongoza watu wapo waadilifu na wenye nia njema kwa taifa lakini pia wapo watu ambao ni wasaliti na hawanania njema kwani wanatanguliza masuala binafsi ikiwemo ubadhirifu, rushwa na matendo mengine ambayo si mazuri kwa mwenyezi Mungu na wananchi pia
''Ndugu zangu viongozi wadini ninawaombeni sana kila mmoja bila kujali imani yake amuombee sana rais wetu pamoja na watendaji wa serikali kwa ujumla kwani kuongoza wananchi ni kazi kubwa na tutakwenda kujibu kwa Mungu iwapo tutafanya vibaya kwani mimi naamini serikali iliyochaguliwa na watu imewekwa na Mungu mwenyewe''
mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa taasisi za kidini kwa muda mrefu zimekuwa zikisaidia juhudi za serikali katika kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi jambo ambalo pia linasaidia utekelezaji wa Ilani ya chama tawala inayoongoza serikali.
“ninaendelea kuzishukuru taasisi za kidini kwa kuisaidia serikali katika kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi kwani kwa upande wa sekta ya afya mkoa una zahanati kumi, vituo vya afya vinane na Hospitali mbili zinazomilikiwa na taasisi za kidini na nimeniambia kuwa mnaendelea na ujenzi wa vituo viwili vya afya ambavyo vikikamilika vitaongeza upatikanaji wa huduma,” alisema
Aidha alitoa mchango huo kwa lengo la kuzindua harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya katika siku ya maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika Kimkoa katika Kijiji cha Kabwe, Kata ya Kabwe wilayani Nkasi ambapo alikuwa rasmi katika sherehe hizo.
Hata hivyo aliwashukuru waumini wa madhehebu mbalimbali  kwa kuendelea kuiombea serikali na kusisitiza kuendelea kuhubiri amani iliyopo ili nchi isonge mbele katika sekta zote na wananchi waweze kufurahia amani, utulivu na uhuru wa kuabudu.
Kwaupande wake katibu wa Bakwata mkoa wa Rukwa Mohammed Khatibu alipokuwa akisoma risala mbele ya mgeni rasmi alisema kuwa Baraza hilo linahitaji kiasi cha shilingi 6,910,000 ili kuweza kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya ambacho kipo katika hatua ya upauaji.
“Tunaendelea na ujenzi wa kituo cha afya kilichopo kirando Nkasi ambacho kwa sasa kipo katika hatua ya kupaa na mahitaji yetu ni kupata bati za futi 8 bando 11 zenye thamani ya shilingi milioni 2.97, mbao 500 za kupiga kenchi ambapo jumla kuu nivshilingi  6,910,00 ikiwemo pamoja na malipo ya fundi  na misumari.

Mwisho

No comments:

Post a Comment