Saturday 4 November 2017

Waziri aagiza kutimuliwa kazi walimu wanaofanya Mapenzi na wanafunzi wao

Na Gurian Adolf
Katavi
Naibu Waziri wa  nchi  Ofisi ya rais Tamisemi George  Kakunda  ameuagiza uongozi wa Serikali ya wilaya ya Mpanda  Mkoani  Katavi kuwafukuza kazi  walimu walio na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao. 
Naibu waziri huyo alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na Madiwani wa  halmashauri ya wilaya ya Nsimbo  pamoja na watumishi wa halmashauri hiyo  katika ukumbi wa mikuto wa halmashauri hiyo.
 Kabla ya kutoa agizo hilo Diwani wa  Kata ya Katumba  Seneta  Baraka  alimweleza  Naibu Waziri Kakunda  kuwa  yeye  kama  Diwani  maisha yake  yako  hatarini  kutokana na kuwafatiliwa na walimu wanaofanya  mapenzi na wanafunzi wao. 
Alisema kumekuwa na tabia sugu kwa baadhi ya walimu wa  Shule mbili za  Sekondari  katika Makazi ya  Wakimbizi ya  Katumba ya kufanya mapenzi na  wanafunzi wao na  wengine kuwaoa kwa madai kuwa walimu kufanya  mapenzi na  wanafunzi wao ndio  ruzuku yao.
Diwani huyo alisema amekuwa amekuwa akipata  ushirikiano  mdogo kutoka  kwa uongozi w  wilaya licha yeye kutoa taarifa za tabia  hiyo lakini hakuna  hatua zilizochukuliwa licha ya kuwepo kwa ushahidi  na  matokeo yake  yeye ndio amekua akitishiwa maisha.
Diwani  Seneta  alizitaja shule  za  Sekondari ambazo  baadhi ya walimu wake wanatabia ya kufanya ngono na wanafunzi wao kwa kisingizio cha kuwa ni  ruzuku kwao kuwa ni  Katumba  Sekondari pamoja na  Kenswa  Sekondari.
Seneta  alilifafanua kuwa  yupo mwalimu mmoja ambaye aliamua kumwoa  kabisa mwanafunzi wake na swala  hilo alishalizungumza  kwenye baraza la  madiwani lakini hakuna  hatua zilizochukuliwa na  badala yake  baadhi ya  madiwani wenzake  wamekuwa ndio wakwanza  kuwafikishia taarifa walimu kuwa  yeye  ndio anae shupalia  jambo hilo.
 Alisema kuwa mwalimu  mmoja  baada ya penzi kukomaa na mwanafunzi wake aliamua kmuoa  kabisa  na  wanaishi nae na  aliamua kupeleka  mahali kwa  wazazi wake  hata  hivyo  mama  mzazi wa  mwanafunzi huyo alikataa  kupokea  pesa za mwalimu  huyo.
 Alimwomba  waziri Kakunda amsaidie ili aweze kupatiwa ulinzi kwani vitisho anavyo pata vinahatarisha maisha yake  na  ndio maana siku hizi  amepunguza  hata kutembelea  kwenye maeneo ya  starehe kwa kuhofia maisha yake.
Mara baada ya kupokea  maelezo  hayo  naibu Waziri   aliungiza uongozi wa  Serikali ya wilaya ya Mpanda  kuhakikisha inawachukulia  hatua walimu hao maramoja  ikiwemo kuwafukuza kazi
 Alisema sheria  inakaza kufanya mapenzi  na  mtoto  mwenye umri  chini ya miaka 18 hivyo wanaofanya hivyo watambue kuwa wanafanya makosa  na wala  hakuna kusingizia kuwa  walikubaliana .
Kakunda alisema lengo la  Serikali ni  kuhakikisha mtoto  anasoma  kuanzia  darasa la  kwanza hadi kidato cha  nne  hivyo  aliwaonya wanaowaozesha wanafunzi wakae  chonjo  kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Alizitaka  kamati za ulinzi na usalama za  Kata  nchi nzima zishirikiane kufanya kazi ya kuhakikisha  zinadhibiti  mimba za wanafunzi kwenye  kata  zao.
Kwaupande wake ofisa  elimu Sekondari ya  halmashauri ya  wilaya ya Nsimbo  Said Malamba  alisema kuwa  swala  hilo tayari amekwisha anza kulishughulikia.
 Alisema  tayari  walmu wawili wa  shule  ya  Sekondari ya Katumba na mmoja  wa Seokndari ya Kenswa  walisha andikiwa  barua na   tume ya utumishi ya kujieleza  kutoka na tuhuma  hizo na baada ya kujieleza tayari mwalimu  Mmoja  wa  Shule ya  msingi  Katumba  mwalimu  ambaye ni mwalimu Fransis  Manyala  amechukuliwa  hatua  na  walimu  wawili  hawakupatikana na hatia.
Alisema  mwalimu  huyo   aliyepatikana  na  hatia tume ya utumishi ya  wilaya ya  Mpanda  amekata  rufaa  kwenye  tume ya utumishi Taifa baada ya kutoridhika na maamuzi ya kusimamishwa kwake kazi.
Mwisho

No comments:

Post a Comment