Tuesday 10 October 2017

Mvua yaleta maafa

Na Gurian Adolf
Kalambo
KAYA 11 zimabaki bila makazi baada ya mvua kubwa kunyesha na kuezua nyumba katika kijiji cha Matai asilia kata   ya Matai wilaya ya kalambo mkoani Rukwa.

Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa kijiji hicho Isack  Sawala alisema tukio hilo likitokea jana baada ya mvua kubwa kunyesha ikiambatana na upepo mkali.
Alisema kuwa hakuna mtu aliyefariki duninia kufuatia tukio hilo lakini wapo baadhi yawatu walio jeruhiwa nakukimbizwa  katika kituo  cha  afya  cha  Matai  kwa  ajili  ya  matibabu.

Naye Katibu tawala wa wilaya hiyo  Frank  Sichalwe alisema kuwa nyumba 8 zimeboka kabisa nahazifai kabisa kuishi tena binadamu na wananchi hao wanahitaji msaada wa hali namali.

Alisema kuwa  kamati ya maafa ya wilaya hiyo inaendelea na jitihada zakuwasaidia wananchi hao ambao wanakabiliwa na hali ngumu kutokana na tukio hilo.

Aidha alitoa wito kwa wananchi wenye mapenzi mema kutoa misaada ya kiutu ilikuwasaidia wananchi hao kwani wanahitaji hifadhi kwaajili yao na mali zao kwakuwa hawana makazi ya kuishi. 

Hata hivyo alitoa wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanajenga nyumba kwakutumia cement tofauti na sasa ambapo baadhi ya wananchi wamejenga nyumba zao kwa kutumia udongo wa hawaida hali inayosababisha nyumba hizo kutokuwa imara.

Mwisho

No comments:

Post a Comment