Wednesday 11 October 2017

Meya azushiwa jambo

Na Walter Mguluchuma
Katavi
Meya wa  Manispa ya  Mpanda  Willy  Mbogo  amekanusha  uvumi unaoenea katika  maeneo mbali mbali ya Mkoa wa  Katavi  kuwa ameanza mikakati ya kumng'oa mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastian Kapufi katika uchaguzi mkuu ujao
 Mbogo  ambae  ni  Diwani wa  Kata ya  Kashauli  kupitia CCM  alisema hayo jana   wakati akiwahutubia   wananchi wa  Kata ya  Majengo katika uzinduzi wa  kisima cha maji kilichojengwa na  Kampuni ya kuuza  mafuta ya GBP  kilichogharimu kiasi cha  shilingi  Milioni 55 ikiwa ni  msaada  uliotolewa  na  Kampuni  hiyo.
Alisema  kuwa amekuwa akizushiwa kuwa anampango wa kugombea  ubunge  katika  Jimbo hilo kitu ambacho sikweli kwani mpaka sasa hana mpango wowote wakugombea ubunge katika jimbo lolote mkoani humo.
 Alisema  kuwa yeye binafsi anapenda  kuwahakikishia  wakazi wa  Manispaa ya  Mpanda  na  wananchi wa  mkoa wa  Katavi kwa ujumla kuwa hana  mpango wa kugombea  ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wa  2020  kwenye  jimbo  lolote la  Mkoa wa  Katavi.
 Alisema kuwa  nafasi ya udiwani  aliyonayo  inamtosha hivyo  ataendelea kuwatumikia  wananchi katika nafasi  hiyo kwani inamfanya kila  siku kufanya kazi ya kuwatumika wananchi kwa  karibu  zaidi.
"nimekuwa  nikuzushiwa  mara  kwa  mara  kuwa  nampango wa kugombea  udiwani,hata  hivi karibuni  wakati wa  mkutano  mkuu wa  CCM  wa Wilaya ya  Mpanda  baadhi ya  wajumbe wa mkutano huo walihoji  swala  hilo" alisema
Alisema  ameamua  kukanusha  mapema  kwani  anaona  siku  hadi  siku  watu wanaendelea kuzusha  kitukisicho moyoni  mwake kwa  sasa wala  hafikikii  kabisa zaidi ya  kuendelea kuwatumukia  wananchi wake kwa  nafasi ya udiwani.
 Alieleza kuwa  wakati wa  mkutano Mkuu wa  uchaguzi uliofanyika   yeye  aligombea  ujumbe wa  mkutano  mkuu wa Taifa  na    alishinda hivyo watu  ambao  walikuwa  wameanza kumzushia  kuwa  kwanini   agombee  nafasi hiyo wakati pia  anampango wa kugombea  ubunge kwenye  uchaguzi  mkuu   ujao.
Mwisho

No comments:

Post a Comment