Saturday 2 September 2017

TRA Rukwa yafanya msako wa magari

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MAMLAKA ya mapato TRA mkoani Rukwa jana imefanya msako maalumu kwalengo la kukagua mabasi ya abiria pamoja na ya mizigo ambayo hayajalipiwa kodi mbalimbali pamoja nakuangalia kama wanachukua risiti za EFD pindi wanapojaza mafuta Katika vituo vinavyouza mafuta mkoani humo. 

Msako huo ulianza majira ya saa 11:30 za alfajiri Katika stendi kuu ya mabasi iliyopo mjini Sumbawanga ambapo walianza kuyakagua mabasi yanayotoka mjini Sumbawanga na kuelekea katika wilaya za mkoa huo  pamoja na mabasi yanayokwenda Katika mikoani.

Akizungumza wakati akiongoza msako huo Meneja msaidizi idara ya ukaguzi wa TRA mkoa huo, Amina Shamdas alisema kuwa mamlaka hiyo inashirikiana na kampuni ya Yono Auction Mart kufanya ukaguzi huo.

Alisema kuwa mamlaka hiyo ilibaini wafanyabiashara wa usafirishaji wamekuwa hawadai lisiti zinazotolewa na mashine za EFD wakati wakinunua mafuta pia Magari mengi yana stika za kulipia Mapato za kughushi ndiyo sababu waliamua kufanya msako huo. 

Alisema kuwa kufuatia msako huo anaamini kuwa wafanyabiashara hao watabadirika nakuanza kufuata sheria zilivyo ili waweze kuepukana na mkono washeria vinginevyo watajikuta katika wakati mgumu pindi wanapofanya biashara zao. 

Meneja huyo msaidizi wa idara ya ukaguzi ya TRA mkoa wa Rukwa alisema kuwa ifike wakati kila mwananchi aonefahari kulipa kodi kwani kwa kufanya hivyo atakuwa ametimiza wajibu wake kwa taifa na hatopata usumbufu wowote katika shughuli zake. 

Naye David Philipo mwakilishi wa kampuni ya Action Mart ya mjini Sumbawanga alisema kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa kutoka kwa wafanyabiashara hao ambapo baadhi yao wamekuwa ni wakaidi katika kutii sheria.

Alisema kwakuwa wamejipanga vizuri kwa kushirikiana na TRA watahakikisha hakuna mapato yatakayo potea kwani nilazima serikali ikusanye kikamilifu ili iweze kuwahudumia wananchi wake. 
Mwisho

No comments:

Post a Comment