Na Gurian Adolf
Sumbawanga
Katika kuhakikisha Kuwa mkoa wa Rukwa na taifa Kwaujumla unafanikiwa kupitia Ziwa Tanganyika wadau waviwanda mkoani Rukwa wameishauri serikali ya mkoa huo kutangaza bandari ya Kasanga Kuwa lango la kiuchumi ili nchi inufaike kupitia mataifa yanayotumia Ziwa hilo
Wakizungumza Katika kikao maalumu kilichowakutanisha wadau wa viwanda kutoka Katika halmashauri za mkoa huo walisema Kuwa Kwa kupita bandari hiyo mkoa huo na taifa Kwa ujumla utanufaika iwapo mataifa hayo yataitumia bandari ya Kasanga Kwa kupitishia bidhaa zao.
Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo Ally Kasanda alisema Kuwa kuwepo Kwa bandari hiyo ni fursa ambapo mataifa ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Burundi na Zambia yataitumia kupitishia mizigo yao pindi wanapoipokea Katika bandari ya Dar es salaam.
Alisema Kuwa nchi hizo hazijapakana na bahari hivyo Kama zikisafirisha mizigo kutoka mataifa ya magharibi kupitia bahari ya hindi na kuishusha Katika bandari ya Dar es salaam na kisha kuisafirisha Kwanjia ya nchi kavu mpaka mkoani Rukwa natena kuifikikisha Katika bandari ya Kasanga kisha kuisafirisha kwanjia ya maji kupitia Ziwa tanganyika mpaka katika nchini zao.
Kasanda alisema Kuwa iwapo mkoa wa Rukwa wataiboresha bandari hiyo watafanikiwa na nchi itapata mapato mengi kwaniwatalipa tozo mbalimbali na kisha wananchi ambao watawekeza Katika sekta ya viwanda wataweza kusafirisha bidhaa zao Kupitia bandari hiyo na kufanya biashara ya kimataifa.
Naye Mbunge wa viti maalumu mkoani Rukwa Bupe Mwakang'ata aliishauri shirika la umemeTanesco,mkoani Rukwa kuhakikisha linaongeza kasi katika kuwafikishia wananchi wa vijijini umeme ili nao waweze kunufaika na nia ya serikali Katika kuhakikisha Kuwa wananchi wake wanamiliki viwanda kwani bila nishati ya uhakika ya umeme suala la viwanda litakuwa ni hadithi.
Alisema Kuwa wananchi hawanabudi kunufaika na awamu hii ya tano kwakuwekeza Katika viwanda ili waweze kujikomboa kiuchumi na kuzalisha ajira ambazo zitawanufaisha wakazi wa mkoa huo.
Kwaupande wake katibu tawala wa mkoa wa Rukwa Bernard Mkali alisema Kuwa mkoa huo unajumla ya viwanda 950 na alitoa wito kwawananchi wa mkoa huo kuwekeza zaidi katika viwanda iliwaweze kufungua fursa ya kiuchumi Kwa wakazi wa mkoa huo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment