Wednesday 12 July 2017

Kisima cha maji kuimarisha ndoa

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
WAKAZI wa vijiji vya Kalepula A na B kata  ya  ulumi  wilaya  ya  kalambo mkoani  Rukwa  wamelazimika kufanya sherehe kwa siku nzima baada ya  kuondokana  na  tatizo  la  maji  lililo dumu tangu kuanzishwa  kwa kijiji hicho zaidi  ya miaka  20 baada ya serikali  wilayani  humo kuchimba kisima  cha  maji  kilicho  gharimu   kiasi  cha  shilingi milioni  50.
Kabla ya kuchimbwa kisima hicho wananchi  hao walikuwa wanalazimika  kutembea umbali wa zaidia ya kilomita tano  wakitafuta maji  huku   wakina mama wakilazimika  kuamka  majira   ya  saa  tisa za usiku kwa lengo la  kutafuta maji hayo.
Wakiongea  kwa nyakati tofauti wakati  wa sherehe hiyo ya  kufurahia kisaima hicho, wananchi  hao  wamesema  ujezi  wa  kisima   hicho  umewasaidia kuondokana na   tatizo la  maji  na  kuiomba serikali  kuwasambazia  haraka  katika nyumba zao ili  wanze  kuyatumia  maji hayo.
Lucia Katata mkazi wa kijiji cha Kalepula A alisema kuwa wameteseka kwa muda mrefu kwa kuamka nyakati za alfajiri kwa lengo la  kutafuta maji, huku wengine ndoa zao zikivunjika na baadhi kupata kipigo kutoka kwa wenzi wao walikuwa wakiwatuhumu kutumia kisingizio cha kutafuta maji na kusaliti ndoa zao.
Ofisa mtendaji  wa  kata  hiyo  Michael Mazila, alisema kuwa kisima  hicho  kilinza kuchimbwa  mwaka  2015 lakini kutokana na ujenzi wa kusua sua baadhi ya   watu walichukia na kuamua kukifukia kwa hasira nyakati za usiku huku wakidai kuwa mkandarasi aliyepewa zabuni ya kuchimba kisima hicho hana nia ya kuwatoa katika dhiki waliyo nayo. 
Kutokana na kitendo hicho mkandarasi alianza kukifukua upya kisima hicho  na kulazimika kuajiri walinzi ambao walikuwa wakilinda kwa wakati wote mradi huo ukiwa unatekelezwa.
Alisema kuwa ili kisima hicho kiwe  endelevu na kitoe maji kwa muda mrefu wananchi wanaoishi  karibu na kisima hicho wamepigwa marufuku kufanya shughuli za kilimo karibu na kisima hicho hivyo niwajibu wao kuheshimu utaratibu  huo.
Kwa upande wake diwani  wa  kata  hiyo Modest  Tuseko alisema kuwa mbae wananchi walikuwa wakiteseka kwa kukosa huduma ya maji safi na salama, huku wakipatwa na magonjwa ya milipuko ikiwemo homa ya matumbo kutokana na kutumia maji yasiyo safi na salama.
Alisema kuwa hivi sasa hatua inayofuata ni kusambaza maji katika nyumba za wakazi wa kata hiyo ili kuwaondolea adha  ya kutembea umbali mrefu kufuata maji kwani baadhi ya nyumba zipo umbali mkubwa kutoka kilipo  kisima hicho.
Mwisho

No comments:

Post a Comment