Sunday 16 July 2017

Aesh aiagiza Manispaa ya Sumbawanga iwalipe fidia wakazi wa Chanji watakao vunjiwa nyumba zao

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
LICHA ya halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa kutangaza kutolipa fidia kwa wakazi wa Chanji ambao watapisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami utakaojengwa kati ya Majengo hadi Chanji katika mji wa Sumbawanga, mbunge wa jimbo  la  Sumbawanga mjini Aesh Hilary ameagiza kuwa ni lazima watu hao walipwe fidia na yeye yupo tayari kusimamia kwani hayupo tayari kuona mwananchi  anavunjiwa nyumba yake bila kulipwa  fidia.
Mbunge wa jimbo la  Sumbawanga Aesh Hilary akiwahutubia wakazi wa Chanji mjini Sumbawanga

Agizo hilo alilitoa jana  katika eneo la  Soweto Chanji wakati akihutubia mamia  ya watu waliojitokeza kumsikiliza alipokuwa akizungumza na wananchi wa Chanji ambapo pia alitumia fursa hiyo kujibu kero mbalimbali za wananchi wa eneo hilo.
Moja kati ya kero zilizo wasilishwa kwa mbunge huyo ni malalamiko ya baadhi ya wananchi ambao watavunjiwa nyumba zao kwa madai kuwa wanapaswa wapishe ujenzi wa barabara itakayo jengwa kwa kiwango cha lami kutokea  Majengo mpaka kuunganisha na barabara iendayo mkoani Mbeya.
Alisema kuwa sio haki  kumvunjia mwananchi  nyumba yake hata kama itakuwa ni sehemu ya nyumba ni lazima alipwe fidia na yeye mwenyewe atasimamia kwani hayupo tayari kuona mtu  anavunjiwa nyumba bila kulipwa fidia yoyote.
Wakazi wa Chanji Soweto mjini Sumbawanga wakimsikiliza mbunge wao Aeshi Hilary

Mbunge huyo alisema kuwa kitakua sio kitendo cha uungwana kuvunja nyumba ya mwananchi  bila kulipa fidia, alisema kuwa ni lazima halmashauri ya Manispaa itafute fedha za kulipa fidia naye atahakikisha wananchi hao wanapatiwa haki  yao.
Alisema kuwa maendeleo ni kitu kizuri lakini pia lazima haki  itendeke na si kuwatia  hasara watu wengine kwa sababu ya ujenzi wa barabara kwani walitumia  fedha zao wakati wa ujenzi wa nyumba hizo na si busara kuvunja halafu wasilipwe fidia.
"Ndugu zangu ninani  ambaye wangekuwa tayari kuvunjiwa hata sehemu ya nyumba yake bila kulipwa  fidia kwa madai kuwa tunajenga barabara?, naamini hakuna sasa iweje wananchi hawa wa Chanji wao wasilipwe fidia...nitahakikisha wanapata  haki  yao kwani Mimi mbunge wao sipo  tayari kuona hilo"... Alisema Hilary.
Kuhusu suala la  kulima karibu na vyanzo vya maji alisema kuwa katika hilo hayupo tayari kuunga mkono ni lazima sheria ifuatwe wanaolima bustani wanapaswa kuacha umbali wa mita  6o kwani ndivyo  sheria inavyo  elekeza na nilazima  iwe hivyo vinginevyo vyanzo vya maji vitakauka na wananchi watapata shida ya maji.
Aidha aliwasihi wananchi wa eneo hilo kuheshimu sheria za nchi na iwapo kuna jambo ambalo  hawaridhiki nalo waende ofisini  kwake kwani yupo yeye mbunge wao ambaye yupo kwaajili ya kuwasaidia katika changamoto mbalimbali na iwapo hawata mkuta  yeye yupo katibu  wake na atawasikiliza na kuwasiliana na mbunge wao kisha  ufumbuzi wa tatizo lao utapatikana.
Mwisho

No comments:

Post a Comment