Thursday 22 June 2017

Marufuku kuvua,kuoga ziwani

Na Gurian Adolf
Kalambo
HALMASHAURI ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imepiga maruku shughuli za uvuvi wa samaki pamoja na kuogelea katika ziwa Tanganyika mpaka hapo idara ya afya wilayani humo itakapo toa taarifa ya kumalizika kwa ugonjwa huo.
Uamuzi huo umefikiwa kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa  ugonjwa wa kipindupindu   kwenye kijiji cha Samazi kilichopo  mwambao wa ziwa hilo ambapo kijiji hicho kinakaliwa na wavuvi zaidi.
Akizungumzia marufuku hiyo Afisa uvuvu wa wilaya hiyo Wilbroad Kansapa alisema kuwa wavuvi ambao wamekuwa walifanya shughuli zake katika ziwa hilo wako hatarini kupata ugonjwa huo kutokana na kutochukua tahadhari ya kutosha kwani baadhi yao wamekuwa wakinywa na kuoga maji  hayo kitendo ambacho ni hatari.
Alisema kuwa baadhi ya wavuvi na waogeleaji wanapokuwa wakifanya shughuli hizo katika ziwa hilo na kujikuta wakinywa maji kitendo ambacho ni hatari kwani hawawezi kujua kama Maji hayo yana vimelea vya ugonjwa huo.
Mpaka hivi sasa watu 18 wamekwisha ugua  ugonjwa  huo    na ni mtoto  mmoja aliyefahamika kwa jina la Lina Protas(5) ndiyo aliyefariki dunia kwa ugonjwa huo na idara ya afya wilayani humo inafanya kila liwezekanalo katika kuhakikisha kuwa wanakabiriana na kasi  ya kuenea kwa ugonjwa huo katika halmashauri hiyo.
Afisa uvuvi huyo alisema kuwa wanajitahidi pia kudhibiti wavuvi kutoka katika nchi  jirani ya   Zambia  hususani  katika  maeneo  ya  Mpulungu  na  Mbala ambao wanafika mpaka upande wa nchini Tanzania maeneo ambayo yana kipindu pindu  kufanya shughuli za uvuvi ili kuzuia wasije pia wakapata ugonjwa huo na kuupeleka nchini mwao na hivyo kusababisha watu kuugua.
Kwa upande  wake  afisa  uvuvi wa kata ya Samazi ambako  mpaka hivi sasa ndio kuna ugonjwa huo Medadi Hosea alisema kuwa kwa   kushirikiana na viongozi wa  serikali za vijiji vilivyopo katika kata hiyo wameweka sheria ndogo kuwa iwapo akikutwa mvuvi anavua samaki ama akiogelea ndani ya ziwa hilo atakamatwa na kulioishwa  faini  ya  shilingi  elfu 50,000.
Hata hivyo kuibuka kwa ugonjwa wa kipindu  pindu  katika kijiji hicho cha Samazi kumeonekana kumnyima raha mkuu  wa mkoa wa Rukwa Zelote Steven ambaye amaonekana kuwa karibu na wilaya hiyo zaidi kwa kufanya ziara na mikutano ya kutoa  elimu katika kuhakikisha kuwa ugonjwa huo unadhibitiwa ili usienee katika sehemu nyingine huku akizingatia agizo la  raisi John Magufuli kwa wakuu wa mikoa hapa nchini kuwa hataki kusikia kuwa wananchi wanapoteza maisha kwa ugonjwa huo.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment