Wednesday 3 May 2017

Zelote Steven Kuwaongoza wanahabari katika kuadhimisha siku yao

Na Gurian Adolf
Sumbawanga

Leo ni Mei 3, tarehe ambayo imeteuliwa na dunia kwaajili ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani.

Ni siku  muhimu sana katika Tasnia  ya habari siku ambayo wanahabari  wanapata fursa ya kukutana na wadau(wananchi) ili kuweza kuzungumza ama kubadilishana mawazo.

Kubwa zaidi ni kutazama ni zipi changamoto zinazo ikabiri  sekta ya habari pamoja ma watendaji wake na namna gani ya kutatua, lakini pia ni fursa ya wadau wa habari kukaa na kuweza kutoa ya moyoni"kutapika nyongo" kuhusiana na masuala mazima  ya habari.
                                              Zelote  Steven mkuu wa mkoa wa Rukwa
Mkoani Rukwa wanahabari  pia wanaadhimisha siku hii watapata nafasi ya kukutana na baadhi ya wadau wa habari katika ukumbi uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga yaani eneo la  Bomani.

rukwakwanza.blogspot.com itakuwepo katika eneo hilo kwaajili ya kukutana na wadau wa habari maana inafikia wananchi kwa njia ya kisasa inayoitwa online Journalism.

Katika maadhimisho hayo Mkuu wa mkoa wa Rukwa Zelote Steven ndiyo mgeni rasmi, ambapo atafungua kikao ama kongamano baina  ya wana habari na wadau wao.

Ni wakati wa waandishi wa habari kuweza kutafakari ni kwakiasi gani wanaitumikia jamii yao katika kuipasha habari.

Pamoja na changamoto nyingi walizonazo wanahabari  kama kutopewa habari kwa wakati ili waifikishie jamii, ushirikiano duni kutoka kwa tasisi za umma na binafsi, kupigwa na kuumizwa, kutishiwa usalama wa maisha yao, kunyimwa haki zao za msingi, kunyanyasika wao pamoja na familia zao, maslahi duni  kutoka kwa waajiri na hata kuuawa.

Ni ukweli usiopingika kuwa pamoja na changamoto hizo lakini bado wamekuwa wakijitahidi kuihabarisha jamii kadiri ya uwezo wao na Mazingira.

Sasa hivi teknolojia inakua kwa kasi  kubwa na hivyo kuwafanya wana habari kila siku kusoma ili waweze kuendana na kasi ya mabadiriko hayo.

Mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoa wa Rukwa Musa  Mwangoka akizungumza na rukwakwanza.blogspot.com alisema kuwa moja kati ya changamoto kubwa ni jamii na wadau wa habari kutoipa umuhimu makubwa sana tasnia  hii.

Alisema kuwa tasnia ya habari ni tasnia  mtambuka ambayo ili mtu  afanye kazi ya habari ni lazima ahakikishe anasoma kila Mara na kujua mambo mengi.

Akitolea mfano alisema kuwa haimlazimu Daktari kusoma kuhusu masuala ya kiuchumi, kwakua yeye anaweza kujikita katika utabibu tu lakini mwanahabari ni lazima asome  vitu vingi  maana kunawakati atashughurika na masuala ya kiuchumi, afya,elimu, sheria na yote yanayomuhusu binadamu.

Kitu ambacho ni kugumu sana na inampasa maeneo yote hayo hata kama si kubobea lakini walau awe na uelewa wa kawaida.

Hii inatoa changamoto kubwa kwa wanahabari  kukubali kusoma kila kitu na kwa kila wakati.

Ni ukweli usiopingika na wala hawakosei baadhi ya watu kuiona  kama muhimiri wa tatu wa taifa  kutokana na 'unyeti' wake.

Kitaifa siku hii inaadhimishwa jijini Mwanza na Mgeni rasmi atakuwa raisi  wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Kila mkoa umetuma mwakilishi huko ambapo mkoa wa Rukwa Joshua Joel yupo huko kwaajili ya kuwawakilisha wanahabari  wa mkoa wa Rukwa.

rukwakwanza.blogspot.com inawatakia maadhimisho mema  wanahabari  wa mkoani Rukwa, nchini  na Duniani kwa ujumla.

Mwisho

No comments:

Post a Comment