Na Gurian Adolf
Sumbawanga
WANAWAKE wawili wameuawa kwa kukatwa mapanga katika matukio tofauti mkoani Rukwa kutokana na wivu wa kimapenzi na kisha wame zao kujinyonga baada ya kufanya mauaji hayo.
Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi POLYCARP URIO ilisema kuwa katika tukio la kwanza lililotokea katika kijiji cha Msia kata ya Milepa, tarafa ya Mtowisa wilayani Sumbawanga Theresia Seleman(39) aliuwa na mumewake aitwaye PATRICK KIPESA(39) kutokana na wivu wa kimapenzi.
Alisema kuwa siku ya Mei 14, majira ya saa 01:30 asubuhi huko mtuhumiwa huyo alimuua mkewake huyo kwa kumkata na shoka na kisha naye kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani sebuleni kwake.
Kaimu kamanda Urio alisema kuwa chanzo cha kufanya mauaji hayo na yeye kuamua kujiua ni wivu wa mapenzi baada ya mtuhumiwa kuhisi kuwa mkewe anamahusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine ambaye hajafahamika kwa jina mpaka hivi sasa.
Akisimulia mazingira ya mauaji hayo alisema kuwa alimvizia mkewe na kumkata na shoka shingoni na kichwani kisha kumsababishia majerahaha kubwa yaliyopelekea kifo chake.
Katika tukio jingine Kaimu kamanda alisema kuwa siku ya Mei 14 huko katika hospitali ya mkoa Sumbawanga mkoa wa Rukwa msichana Fatuma Yusufu( 22),mkazi wa mtaa wa Shengetela alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Alisema kuwa chanzo cha kifo chake ni kutokana na kukatwa na panga kichwani na mzazi mwenzie kutokana na wivu wa kimapenzi.
Aidha alisema kuwa kabla ya mauti kumfika alifika katika kituo cha polisi kutoa taarifa ya kujeruhiwa akiwa na hali mbaya ambapo alipewa PF3 ili aende akatibiwe na ndipo mauti ilipomkuta akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa Sumbawanga.
Mtuhumiwa alikimbia na kutoroka baada ya kufanya mauaji hayo nakisha naye kwenda kujiua kwa kujinyonga.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi hasa walioko kwenye ndoa kuwa waaminifu kwa wenzi wao na kama ikitokea kuna migogoro ni bora wakaitatua kwa kuwashirikisha hata viongozi wa ukoo na kidini kuliko kuchukua maamuzi magumu ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kosa la jinai.
mwisho
No comments:
Post a Comment