Sumbawanga
WAKULIMA wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wameshauriwa kuhudhuria mafunzo yanayotolewa na tasisi zinazotoa elimu wilayani humo kwani fedha zinazotolewa kwaajili ya mafunzo hayo nyingine ni mikopo ambayo serikali inakopeshwa na italipwa na wajukuu wao na wasipo hudhuria na kuelewa vizuri watakuwa wanatenda dhambi ya kuwasababisha wajukuu zao kuja kulipa mikopo ambayo haikuwanufaisha babu zao.
Hayo
yameelezwa na Gibson Haonga meneja mradi wa MIVARF taasisi ambao inaipa
fedha tasisi ya BRENT iliyopo wilayani Sumbawanga ambayo inatoa elimu
ya kilimo cha kisasa cha mpunga ili wakulima wa mpunga waweze kulima
kisasa na hatimaye wapate tija.
Moja ya shamba darasa la mpunga ilililosimamiwa na tasisi ya Brent ambayo ni mbegu aina ya SARO 5
TXD-306 lililopo katika kijiji cha Milepa wilayani Sumbawanga.
Alisema
kuwa mradi wao unapata mikopo kutoka mashirika ya IFAD na Benki ya
Afrika (ADB) ambazo zinatumika kutoa elimu kwa wakulima wa mpunga
wilayani humo lakini wapo baadhi ya wakulima wamekuwa wakitegea
kuhudhuria mafunzo hayo hali ambayo ni kusababisha hasara kwani mikopo
hiyo italipwa hata kama ni baada ya miaka 40 ijayo na wajukuu wao hivyo
ni dhambi kuwafanya walipe mikopo ambayo haikuwanufaisha babu zao.
Haonga
alisema kuwa ni suala la aibu kuona wakulima wanabembelezwa kupata
elimu wakati ni kwa faida yao kwani atakae nufaika na mazao hayo ni
mkulima mwenyewe hivyo kupiga chenga kuhudhuria mafunzo ni kitendo
kibaya kwani wanajikomoa wenyewe na wajukuu wao.
Alisema
kuwa Tasisi ya MIVARF imepata fedha hizo ambazo zitalipwa baada ya
miaka mingi sasa kunahatari kubwa huenda lengo lisifikiwe kutokana na
wakulima kutotaka kushiriki kikamilifu katika mafunzo ya nadharia na
vitendo na hivyo kuendelea kuwaacha wakulima hao wakibaki ni masikini
kwakuwa elimu waliyopewa haikuwakomboa.
Baadhi ya wakulima wanaopata mafunzo kupitia tasisi ya Brent wakiwa wanavuka mto kwaajili ya kwenda kwenye mafunzo katika shamba darasa lililopo katika kijiji cha Milepa wilayani Sumbawanga
Mmoja wa
wakulima anayepata mafunzo yanayotolewa na tasisi ya Brent, Isaya Katepa
alisema kuwa tatizo lililopo hususani katika mafunzo kwa vitendo ni
wakulima kutotaka kwenda kushiriki katika shughuli za mashamba darasa
wakigomea wakidai kuwa wao wanalima mashamba yao binafsi kwahiyo hawana
muda wa kwenda kulima katika mashamba darasa ambayo yameandaliwa
kwaajili ya mafunzo.
Awali
afisa ufundi na elimu wa tasisi ya BRENT inayopokea fedha kutoka katika
mradi wa MIVARF kwaajili ya kuwajengea uwezo wakulima wa mpunga kwa njia
ya mafunzo wilayani humo Faustina Kalyalya akizungumza katika shamba
darasa lililopo katika kijiji cha Milepa wilayani humo ambapo walikuwa
wakiadhimisha siku ya mkulima wa zao la mpunga alisema kuwa tasisi hiyo
ilianzishwa wilayani humo zaidi ya miaka mitano ililiyopita ikiwa na
lengo la kutoa elimu kwa wakulima katika suala zima la kilimo bora
sambamba na kuongeza thamani katika mazao yao.
Alisema
lengo la tasisi hiyo ni kutoa elimu kwa njia ya nadharia na vitendo kwa
wakulima ili wakulima wa mpunga waweze kupata tija kwa kulima kisasa na
kuacha kulima kilimo cha kizamani bila kufuata taratibu za kilimo
bora hali ambayo inawasababisha kupata tija na kuupiga teke umasikini
kutokana na elimu ambayo wataipata.
Baadhi ya wakulima wa mpunga wakiwa wamekaa wakimsikiliza kwa makini mkufunzi wakati wanapatiwa mafunzo ya namna bora ya kulima mpunga kisasa ili wapate tija.
Kalyalya
alisema kuwa lengo kubwa la kutoa elimu kwa wakulima hao ni kuona
wanafanikiwa ambapo ni matarajio ya tasisi hiyo kuwa kila mkulima aweze
kuvuna kwa kiwango cha gunia 40 za mpunga kwa hekari moja hali ambayo
itawawezesha kuona faida katika kilimo wanacholima.
Alisema
iwapo wakulima watafuata utaratibu za kilimo na kufuata maelekezo ya
wakulima hakuna muujiza kuwa watabadirisha maisha yao kutokana na tija
watakazopata kutokana na kilimo cha mpunga ambacho ni ndicho
kinachotegemewa katika bonde la ziwa Rukwa.
Naye
Afisa kilimo wa Wilaya ya Sumbawanga Habona Kwileluya alisema kuwa
iwapo wakulima hao wakitumia mbegu ya mpunga aina ya SARO 5 TXD-306
ambayo inaonekana kufanya vizuri katika bonde hilo watanufaika vizuri
kwani asilimia kubwa ya wakazi wa bonde hilo ni wakulima wa mahindi
pamoja na mpunga.
Baadhi ya wakulima wanaopata mafunzo kupitia tasisi ya Brent
wakimsikiliza afisa kilimo wa wilaya ya Sumbawanga vijijini Habona
Kyileluya
Alisema
kuwa nivizuri wakulima wakafuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo
waliopo katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kulima kwa wakati na
matumizi ya pembejeo za kilimo tofauti na hivyo wasitegemee muujiza wa
kupata mafanikio katika kilimo.
Katika
msimu wa kilimo unaoisha hivi sasa tasisi ya Brent imeanzisha mashamba
darasa katika vijiji vya Ng'ongo, Kaoze, Ilemba, Sakalilo na Milepa
pamoja na kwa vikundi vya wakulima vilivyopo katika bonde la ziwa
Rukwa ambayo wamekuwa ni mfano kwa wakulima hao ili waweze kujifunza
kilimo cha kisasa cha mpunga.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment