Na Gurian Adolf
Sumbawanga
JUMUIA
ya maendeleo mkoa wa Rukwa(JUMARU) hivi karibuni imefanya ziara
katika nchi jirani ya Zambia katika mji wa Mbala kwa lengo la kwenda
kujionea na kujifunza kuhusiana na uhifadhi wa mambo ya asili na
utamaduni.
Ujumbe wa jumuia
hiyo ukiongoza na katibu Mkuu wake wa Taifa Anatory Sikulumbwe
ulifanikiwa kwenda katika nchi hiyo ya jirani kwa kusaidiwa na serikali
ya nchi yetu kwa msaada wa Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dkt Khalfan
Haule ambaye alifanya jitihada za kuwasiliana na serikali ya Zambia
kupitia Mkuu wa wilaya ya Mbala Kedrick Sikombe ambapo nchi hiyo
iliridhia baada ya kukamilika kwa taraatibu zote za kuingia nchini humo.
Picha ya radi ambayo imekuwa ikitumika na kabila la wafipa kama silaha ya jadi dhidi ya waharifu
Akizungumza na rukwakwanza.blogspot.com
katibu Mkuu wa jumaru taifa alisema kuwa lengo la ziara hiyo
lilikuwa ni kujifunza ni nanmna gani majirani hao wameweza kukusanya,
kuanzisha na kuhifadhi vitu vya jadi na asili ili na kuanzisha
makumbusho ambayo yatakuwa ni kielekezo na historia kwa kizazi cha sasa
na baadae ili vizazi hivyo viweze kutambua ni namna gani mababu zao
waliweza kuvitumia kwa nyakati hizo na pia kuwa kama sehemu ya utalii.
Alisema
kuwa baada ya kufika katika makumbusho hayo waliweza kukuta mambo
mbalimbali ambayo mengine yalichukuliwa kutoka nchini Tanzania kutoka
kwa kabila la walungu na wamabwe na yanahifadhiwa nchini Zambia katika
makumbusho yaliyopo mji wa Mbala na kunufaika nayo kwa watu
kuyatembelea kujifunza na kufahamu historia za mababu zao na hata wa
nchi ya tanzania walivyokuwa wakitumia katika mambo ya tiba za jadi,
silaha za vita vya jadi, kujilinda na matumizi mengine kwa wakati huo.
Picha zilizo hifadhiwa katika makumbusho ya Mbala
Alisema
kuwa walifikia maamuzi hayo kwakua jumuia hiyo inatarajia kuanzisha
makumbusho katika mji wa Milanzi uliopi mjini Sumbawanga ambapo pamoja
na kuhifadhi na kutunza pia makumbusho hayo yatakuwa yakitumika kama
sehemu ya tiba za jadi na tafiti mbalimbali zitakuwa zikifanyika
kuhusiana na mambo ya asili ambapo yatakuwa ni makumbusho ya kabila la
wafipa waliopo mkoani Rukwa.
Sikulumbwe
alisema kuwa mpaka hivi sasa tayari wamekwisha pata eneo la kujenga
makumbusho hayo sambamba na fedha kiasi cha shilingi bilioni 8 ambazo
zitatumika katika ujenzi wa makumbusho hayo ambayo yatakuwa ni makubwa
kutokana na vitu vitakavyo hifadhiwa na shughuli zitakazo kuwa
zikifanyika ili watu waweze kwenda kutembelea kujifunza historia na
kupata tiba za jadi katika eneo hilo.
Picha zilizo hifadhiwa katika makumbusho ya Mbala
Alisema
kuwa taratibu zote zimekwisha kamilika kwa mijibu wa sheria za nchi
ndiyo maana serikali ipo pamoja nao na uzinduzi wa ujenzi wa makumbusho
hayo utazinduliwa rasmi mei 28 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa ni Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dkt Halfan Haule ambaye amekuwa
ni msaada mkubwa kwao katika kufanikisha mipango yote.
Katibu
huyo wa Jumaru Taifa alisema kuwa makumbusho hayo yatakuwa ni fursa
muhimu kwa wananchi sio tu wa mkoa wa Rukwa bali nchi nzima na
kwashughuli za tiba za jadi na sehemu muhimu ya kitalii kwa watalii wa
ndani na nje ya nchi ambapo ni matumaini yake watakuwa wanayatembelea
kwa lengo la kujionea mambo mbalimbali.
Picha zilizo hifadhiwa katika makumbusho ya Mbala
Naye
mwenyekiti wa mambo ya jadi na utamaduni wa kituo hicho Germano Wanchelele almaarufu
kwa jina la mzee Kata ushanga alisema kuwa wao wakiwa wataalamu wa
masuala ya jadi watajitahidi kutoa na kutafuta vitu vya jadi ili
vihifadhiwe humo ili watu waweze kwenda kuviona na kujifunza historia
na mambo mbalimbali ya asili ambayo mababu walikuwa wakiyatumia na
mengine yanatumika mpaka hivi sasa katika kabila la wafipa ili
wajifunze tamaduni za kabila hilo.
Alisema
kutokana na kuwepo kwa makumbusho hayo nchi itanufaika kwani wapo
watakao kuwa ni watalii na wagonjwa ambao watatibiwa kwa tiba za jadi
kutoka maeneo mbalimbali ambao watafika katika makumbusho hayo na hivyo
kuwa msaada mkubwa kwa watu hao ambapo baadhi ya mambo ambayo teknolojia
ya kisasa na kigeni inaweza kushindwa kuyapatia ufumbuzi lakini
yakawezekana katika makumbusho hayo.
Baadhi ya wajumbe wa JUMARU waliokwenda wilaya ya Mbala nchini Zambia
Aidha
Mzee kata ushanga alitoa wito kwa wananchi kupenda kutumia vitu vya
asili kwani tafiti nyingi zinaonesha kuwa havina madhara kama vya
kigeni ikiwemo kemikali zenye sumu na kuwataka watu wote wanao toa tiba
za jadi kujiepusha na masuala ya ushirikina na kupiga ramli
chonganishi ambazo ndiyo zimekuwa zikichafua taluma ya tiba za jadi na
kusababisha kuchukiwa na kuonekana kuwa hazifai.
Kedrick Sikombe mkuu wa wilaya ya Mbala nchini Zambia
Hata
hivyo alitoa wito kwa wataalamu wa jadi kujitahidi kujisajili
serikalini ili waweze kutambulika kihalali na waweze kufanya Kazi zao
bila hofu kwani serikali inafahamu uwepo wao na inawalinda hivyo basi ni
vizuri wakafuata taratibu zilivyo ili kuepuka kuvutana na serikali
kwani wapo kwaajili ya kuisaidia jamii kutokana na changamoto mbalimbali
na si vinginevyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment