Saturday 6 May 2017

Mjukuu amuua bibi yake kwa gobore

Na Gurian  Adolf
Sumbawanga
JESHI la polisi mkoani Rukwa linamshikilia David Sakanyanya(26) mkazi wa Kijiji cha Ilonga, Kata ya Mambwe Nkoswe wilayani Kalambo kwa tuhuma za kumuua bibi yake kwa kumpiga risasi ya bunduki aina ya gobore  baada ya kumnyima mashamba.

Tukio hilo lilitokea Mei 4 majira ya saa 6 mchana wakati bibi yake huyo aliyekuwa akiitwa Sikilieli Nampunje (55) akiwa anarudi kutoka shambani.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Polycarp Ulio alisema kuwa mtuhumiwa huyo alimuua bibi yake kwa kumpiga risasi kutokana na hasira alizokuwa nazo baada ya kumnyima mashamba yake.
kwa mujibu wa maelezo ya mume wa marehemu huyo, Abbas Kapunda alisema mkewe aliuawa na mjukuu wake  huyo akiwa njiani kwenda nyumbani akitokea shambani ambapo alikuwa amekwenda tangu asubuhi kufanya shughuli za shambani.
Alisema kuwa wakiwa kijijini walisikia mlio kwa bunduki ulioambatana na mayowe ya kuomba msaada ndipo yeye pamoja na wananchi wengine walipokimbilia eneo la tukio na alishtuka baaada ya kuona aliyepigwa risasi ni mke wake Sikilieli, na walimkuta  akiwa anagaagaa chini kwa maumivu makali huku akivuja damu nyingi.


Alisema kuwa baada ya kushuhudia tukio hilo aliishiwa nguvu ndipo mashuhuda wengine aliokuwa nao walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ambapo nao uliuaifu uongozi wa kata nao ukatoa taarifa polisi na baada ya muda mfupi askari polisi walifika eneo la tukio.
Baada ya polisi kufika hapo ndipo walipomchukua majeruhi na kumkimbiza  katika Zahanati ya kijiji cha Kalembe,lakini alifariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
  
Mmoja wa ndugu wa marehemu huyo,Moses Alfred alisema kuwa chanzo cha mtuhumiwa kumpiga risasi bibi yake na kumsababishia kifo chake ni kutokana na mgogoro wa mashamba kati yao ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akishinikiza bibi yake huyo amgawie mashamba. 
Alisema kuwa wakati wa uhai wake Sikilieli alikuwa akifuatilia haki yake ya mashamba aliyoachiwa na baba yake mzazi ambaye kabla ya kufariki dunia alimgawa mashamba na yeye baadaye kuwagawia watoto wake,na kubakia na mashamba mengine lakini baadae mjukuu wake  huyo aliyataka na mashamba ya bibi yake  kwa madai kuwa hana uwezo wa kuyalima kwakua amezeeka.

Kwaupande wake mwenyekiti wa Kijiji cha Ilonga, Peter Munga alisema familia hiyo imekuwa katika  mgogoro wa kugombea mashamba kwa takribani miaka mitatu ambapo wajukuu wakitaba bibi yao huyo awepe mashamba na lengo lao ni kuuza mashamba hayo ili wapate fedha.
Kaimu Kaimu Kamanda Urio alisema kuwa mtuhumia yupo katika mikono salama ya jeshi la polisi akiendelewa kuhojiwa na atafikishwa mahakamani mara baada taratibu za kipolisi zitakapo kamilika.
Mwisho

No comments:

Post a Comment