Sumbawanga
SERIKALI imesema kuwa bado nia ya kujenga barabara ya kutoka Wilayani Sumbawanga(bonde la ziwa Rukwa) kwenda wilayani Momba katika mkoa wa Songwe ipo pale pale na hii itajengwa Mara baada ya upembuzi yakinifu pamoja na hatua mbali mbali kukamilika.
Hayo
yamebainishwa na naibu waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano
Bungeni, Mhandis Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la mbunge wa Kwela Ignas Maocha
aliyetaka kujua ni lini serikali itajenga Barabara kwa kiwango cha lami
ambayo ina anzia katika kijiji cha Kibaoni na kupita katika vijiji vya Mfinga,Muze,Ilemba,Kaoze, Kilyamatundu hadi katika Kijiji cha Kamsamba na Mlowo katika wilaya ya Momba mkoa wa Songwe.
Picha ya mbunge wa Kwela Ignas Malocha akihutubia katika mkutano wa hadhara jimboni Kwake katika jimbo la Kwela
Naibu
waziri huyo alisema kuwa bado serikali inania ya dhati ya kujenga
barabara hiyo na ipo katika hatua mbalimbali na hivyo kumtaka mbunge
Malocha pamoja na wananchi wa jimbo la kwela kuwa na subira.
Awali
mbunge Malocha alihoji kuwa ni muda mrefu sasa tangu mikakati hiyo
ilipo anza lakini hafurahishwi na kasi imekuwa ya pole pole kwani barabara hiyo
itakuwa mkombozi kwa wakazi wa bonde la ziwa Rukwa.
Alisema
kuwa iwapo serikali itajenga barabara hiyo itasaidia kufungua bonde
hilo ambalo ni maarufu kwa kilimo cha mahindi pamoja na mpunga na
wananchi wataweza kusafiri kutoka na kuingia wilayani humo bila
usumbufu.
Malocha alisema
kuwa iwapo bara bara hiyo itakamilika niwazi biashara zitashamiri
katika bonde hilo na wawekezaji wataweza kufika na hata kuwekeza viwanda ambayo ndiyo dhamira ya serikali ya awamu ya tamo kwani kutakuwa na
miundombinu ya uhakikaka ambapo serikali pia itanufaika na bonde hilo.
Mbunge
huyo alisema kuwa wakazi wa bonde la ziwa Rukwa wanaisubiri kwa
hamu kubwa barabara hiyo kwani itawanufaisha na wataboresha maisha yao
kwa kuwa wataweza kufanya biashara na watu kutoka maeneo mengine ambao
hawafiki hivi sasa kutokana na kutokuwa na bara bara ya kiwango cha
lami.
Hata hivyo bonde
la ziwa Rukwa iwapo litapata barabara hiyo itasaidia kuinua uchumi wa
mtu mmoja mmoja na taifa kupata manufaa kwa kukusanya Kofi kwani
biashara zitafanyika katika kipindi chote cha mwaka bila kuhofia nyakati
za Masika ambazo zimekuwa na changamoto kubwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment