Friday, 26 May 2017

Dc Nkasi awa mbogo

Na Israel  Mwaisaka
Sumbawanga
MKUU wa wilaya Nkasi mkoani Rukwa Said Mtanda amemjia juu Mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji wa Kisura wa Mil.300 na kuwa atawasioliana na mamlaka husika ili mkandarasi huyo asitishwe kuendelea kuujenga mradi huo ambao amebaini kuwapo na ubabaishaji mwingi.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisura kata ya Nkandasi jana baada ya kuutembelea mradi huo hakuridhishwa na utendaji wa wakandarasi hao na kudai kuwa inaonyesha kabisa kampuni hiyo iliyopewa kandarasi ya kuujenga mradi huo hawana uwezo wa kuifanya kazi hiyo.

alisema kwa jinsi alivyoupitia mradi huo unaonyesha kujengwa chini ya kiwango na umeshindwa kukamilika kwa muda uliowekwa na kuwa mradi huo haujakamilika toka uanze kujengwa kwa zaidi ya miaka sita sasa na kuwa inaonyesha kabisa kampuni iliyopewa kazi hiyo haina uwezo kabisa wa kuujenga mradi huo mkubwa wa manufaa kwa jamii.

Awali Diwani wa kata hiyo Richard Ntemba alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa kampuni ya Mahale Construction Company iliyopewa kazi hiyo imekuwa haitoi majibu halisi ya lini mradi huo utakamilika na kuonyesha wasiwasi mkubwa wa kukamilika kwa mradi huo na kuwa wanahitaji nguvu ya serikali kuhakikisha mradi huo unakamilika hasa baada ya kudumu kwa muda mrefu.

Alidai kuwa Wananchi wa kijiji hicho kero yao kubwa ni maji na walipata matumaini makubwa baada ya kuanza kwa ujenzi wa mradi huo wa maji na sasa furaha yao imetoweka baada ya mradi huo kushuindwa hata kuonyesha dalili za lini mradi huo utakamilika

Kufuatia hari hiyo mkuu wa wilaya alimtaka Mhandisi mshauri wa mradi huo Self Malik kutoka katika kampuni ya O & A kutoa maelezo ya kina mbele ya mkutano huo kueleza nini chanzo cha mradi huo kushindwa kukamilika kwa wakati alishindwa kutoa maelezo ya kina huku msimamizi wa kampuni hiyo ya MAHALE CONSTRUCTION COMPANY Benedict Makungu naye akishindwa kutoa maelezo ya kina ndipo mkuu huyo wa wilaya aliamua kuwatimua Wakandarasi hao mkutanoni kwa madai kuwa hawana tija

Kufuatia hari hiyo aliwataka wasimamizi wa kampuni hiyo iliyochukua kandarasi kuwasiliana na wenye kampuni hiyo kufika mara moja ofisini kwake na kuwakutanisha na watendaji kadhaa wa halmashauri ili waweze kujua tatizo ni nini? na kama hawana maelezo ya kutosheleza waondolewe katika mradoi huo ili waweze kupewa watu wengine wenye uwezo wa kuifanya kazi hiyo na wananchi wakaendelea kupata maji.

Mmoja wa Wanananchi wa kijiji hicho Christina Kaushindo alieleza kwa hisia kali jinsi ambavyo wao wanavyopata shida kubwa ya maji na kuwa wamefurahishwa na jinsi ambavyo mkuu wa wilaya alivyochukua hatua ya kuwaondoa wakandarasi hao mkutanoni na wana amini kuwa hatua stahiki zitachukuliwa ili mkandarasi wa mradi huo aweze kuchukuliwa hatua na mradio huo ukaendelea na wao wakapata maji kitu ambacho ni hitaji lao la siku nyingi.
mwisho

No comments:

Post a Comment