WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WASHIRIKI KIKAO KAZI CHA UTAYARISHAJI WA MPANGO WA MANUNUZI WA WIZARA WA MWAKA 2015/2016 MJINI MOROGORO
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwamini Malemi wa nne kutoka kulia akiwa
pamoja na Wakuu wa Taasisi zote za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
waliohudhuria Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa wizara wa
mwaka 2015/2016 kilichoanza leo katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro, watatu
kutoka kushoto ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi Clodwig
Mtweve, wa pili kushoto ni Kamishna wa Fedha wa Jeshi la Magereza Sanga, waliosimama
nyuma ni baadhi ya Wakurugenzi Wasaidizi wa wizara, Maafisa Bajeti pamoja na Maafisa
Ununuzi wa wizara .
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini
Malemi akisalimiana na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Edwin
Makene baada tu ya kupokelewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi cha wizara
hiyo Manyama Mapesi akielekea kufungua Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa
Manunuzi wa wizara wa mwaka 2015/2016 kilichoanza leo katika hoteli ya Oasis
mjini Morogoro.
Sehemu ya
wajumbe wa Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi wa mwaka
2015/2016 kinachowahusisha Maafisa
Bajeti, Manunuzi, Wakurugezi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Taasisi zote za
wizara hiyo kilichoanza leo katika hoteli ya Oasisi mjini Morogoro , wa kwanza
kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria
na Usajili wa Vyama Marlin Komba, anayefuatia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Sera na Mipango Joyce Momburi na Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na
Uokaoji Maria Kulaya.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini
Malemi akisoma hotuba yake wakati akifungua Kikao Kazi cha Utayarishaji wa
Mpango wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi wa mwaka 2015/2016
kinachowahusisha Maafisa Bajeti, Manunuzi, Wakurugezi, Wakurugenzi
Wasaidizi na Wakuu wa Taasisi zote za wizara hiyo kilichoanza leo katika hoteli
ya Oasisi mjini Morogoro.
Kamishna wa
Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi Clodwig Mtweve akitoa Neno la Shukrani
kwa niaba ya Wajumbe wote wa Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa
mwaka 2015/2016 baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwamini Malemi kufungua Kikao Kazi hizo katika hoteli ya Oasisi mjini Morogoro,
wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manunizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi Manyama Mapesi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini
Malemi wa nne kutoka kulia akiwa pamoja
na Wakuu wa Taasisi zote za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi waliohudhuria
Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa wizara wa mwaka 2015/2016
kilichoanza leo katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro.
No comments:
Post a Comment