TANZANIA KUATHIRIKA ZAIDI NA UHALIFU MTANDAO.
Mazungumzo ya awali kabla ya mkutano wa wanausalama mitandao uliokamilika jijini
Johannesburg nchini afrika kusini yanaweza kusomeka kwa "KUBOFYA HAPA" Mkutano
ambao uliokua na vuta nikuvute kupata suluhu ya changamoto tulizo nazo za
kiusalama mtandao duniani kote zinazoendelea kukua kila kukicha huku ikionekana
dhahiri kabisa wahalifu mtandao wanaelekea kuzidi nguvu huku Tanzania ikiorodheshwa kua ya sita kwa nchi zinazotegemewa kuathirika zaidi na uhalifu mtandao barani Afrika.
Akitolea ufafanuzi wa takwimu hizi Bwana Vernon Frye, Mkuu wa Usalama mitandao wa
kampuni ya Vodacom ya Afrika kusini, alielezea kuhusiana na uhalifu mpya wa
Ransomware ambapo tayari athari zake zimesha onekana Nchini huku aki ibua
mjadala mzito wa wapi tume jikwaa.
Aidha Mjadala mrefu kutoka kwa aliyekua Mkurgenzi wa wakala wa usalama wa Marekani
(National Security Agency – NSA) bwana William Binney pamoja na Raisi na
muanzilishi wa kivinjari cha aina ya Tor kinachotumika sana na jumuia ya wana
usalama mitandao waliibua changamoto ya ufaragha baina ya watumiaji wa mitandao
na namna ya kuendelea kuhakiki kunapatikana uthibiti wa faragha hizi kutotumika
vibaya na wahalifu.
Nikiwasilisha mada ya changamoto tulizo zazo barani Afika na nini kifanyike ili kujikwamua
katika hali mbaya tuliyo nayo hivi sasa ya wimbi la uhalifu mtandao barani
afrika ambapo umeendelea kugharimu bara katika Nyanja za kisiasa, kijamii
pamoja na kiuchumi. Nilielezea kwa kina mambo ya msingi tunayo takiwa kuyafanyia
kazi ili kuhakiki Bara linabaki salama.
Katika mjadala huu ambapo wanausalama mtandao kutoka maeneo mbali mbali ya dunia
waliunga mkono nilicho zungumza kua bado kuna kusua sua katika ushirikiano wa
pamoja katika kutokomeza uhalifu mtandao huwa wahalifu mtandao kuonekana
niwenye ushirikiano ulimkubwa kabisa.
No comments:
Post a Comment