Sunday, 7 June 2015

Mwandishi afunga kituo akidai hafanyi kazi siku ya Sabato

Na Gurian  Adolf
Sumbawanga
WAKAZI wa kijiji cha Ninga B wilayani Kalambo mkoani Rukwa  leo wameshindwa kujiandikisha katatika daftari la kudumu la wapigakura baada ya afisa mwandikishaji kugoma kufungua kituo kwa madai kuwa yeye anaabudu katika dini ya sabato na dini yake haimruhusu kufanya kazi siku ya Sabato.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Pius Benedicto alisema kuwa ilipofika asubuhi kama kawaida wakazi wa kijiji hicho walijitokeza kwa lengo la kujiandikisha, lakini walipofika walikuta kituo kimefungwa.
Alisema baada ya kuhoji sababu za kutofunguliwa kwa kituo hicho walielezwa kuwa mwandishi katika kituo hicho ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi kijijini hapo Dismas Kauzeni hajafungua kituo kwa madai kuwa imani yake ya sabato haimruhusu kufanya kazi siku hiyo.
Mwenyekiti huyo wa kijiji alisema kuwa kutokana na taarifa hiyo wanakijiji hao walimtafuta mwandikishaji mwingine ambaye huwa wanashirikiana katika tukio hilo na alidai kuwa yeye kazi yake ni kutumia mashine tu hususani kupia picha hahusika kwa kazi nyingine.
Kufuatia majibu hayo wananchi wakaanza kuondoka kutoka katika kituo hicho na kurejea majumbani kwao na hivyo kutofanyika kwa kazi hiyo siku ya leo na huenda itaendelea kesho.
Hata hivyo jitihada kuwasiliana na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Kalambo Akilimali Mpozamenye ili kuweza kujua kama halmashauri hiyo inataarifa juu ya tukio hilo na jitihada zilizofanyika ili kulitatua simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment