Sunday 24 May 2015

RUKWA WAANZA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA LEO



Na Gurian  Adolf
Sumbawanga

WAKAZI katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wanaendelea na zoezi la kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura kazi ambayo imeanza tangu majira ya saa 2;00 za asubuhi ya leo.

Watu wamejitokeza katika vituo vya kuandikishia kwaajili ya kujiandikisha ili waweze kupata  fursa ya kushiri uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu ambapo itakuwa ni uchaguzi wa madiwani, wabunge na rais.

 Akizungumza na Ndingala Fm muda mfupi uliopita Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Himid Njovu amesema kuwa mpaka hivi sasa zimejitokeza changamoto ndogo ndogo kama vile mashine kuweka kumbukumbu za mtu aliepita na hivyo kila mara kuzirudia kumbukumbu hizo lakini tayari wamesha tatua hali hiyo.

Kwa mujibu wa Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga amesema kuwa taratibu zote zimekwisha andaliwa na kila mtu mwenye sifa ya kupiga kura atapata fursa hiyo bila hofu yoyote.

Amesema iwapo kutajitokeza changamoto yoyote wamejipanga kukabiliana nayo na katika kituo chochote ambacho kutakuwa na changamoto hiyo watoe taarifa haraka ili kutosababisha kusimama kwa zoezi hilo.

Aidha ameendelea kutoa wito watu kujitokeza ili kujiandikisha kwa lengo la kupata sifa za kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao na hivyo kuchagua viongozi wanaowafaa.









 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 23 Mei 2015  kuelezea juu zoezi la uandikishiaji wa Wananchi kwenye daftari la kudumu la Mpigakura lililoanza rasmi leo tarehe 24 Mei 2015 Mkoani Rukwa. Kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.

No comments:

Post a Comment