Wednesday, 27 May 2015

Majeshi ya Hamas yalaumiwa kwa ukatili

PALESTINA
 
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limelaumu majeshi ya Hamas huko Gaza kwa kuendesha vitendo vya kikatili na utekaji nyara, mateso na mauaji kwa raia wa kipalestina kufuatia mgogoro kati ya Israel na makundi ya wapiganaji wa Palestina katika maeneo ya mpakani.
Mashambulio hayo yaliwalenga raia wakiwatuhumu kushirikana na Israel.
Amnesty imesema kwamba hali ni mbaya wakati vikosi vya askari wa Israel wakiwa katika harakati zao za mauaji ya kutisha na uharibifu kwa watu wa Gaza,Hams inatumia fursa hiyo kujipanga kwa ushindi.
Ripoti hiyo inabainisha kuwa harakati za chama cha Hamas ambacho kimekuwa kikiaminiwa inaonyesha kuwa imekuwa ikitumia mashambulizi ya majeshi ya Israel kulipiza kisasi dhidi ya maadui ndani ya chama hicho.
Wapalestina wapatao 23 kwa mjibu wa ripoti hiyo wameuawa kinyama huku mamia wakifungwa na kuteswa, wakiwemo wanachama wa chama cha upinzani kinachoipinga Hamas chama cha Fatah.
Hamas imekuwa ikiwalaumu maadui zake kuwa wamekuwa wakishirikiana na Israel ambapo ripoti hiyo inabainisha kuwa wengi ya waliouawa ni wale waliokuwa wamefungwa gerezeni wakati wa mgogoro ulioibuka hivi karibuni, ambapo baadhi yao waliuawa kinyama hata kabla ya kesi zao kumalizika.
Katika tukio moja la kushitua wanaume sita waliuawa kwa kupigwa risasi nje ya Msikiti walipokuwa wamepiga magoti mbele ya umati wa watu wakiwemo wanaume wanawake na watoto.
Ripoti hiyo ya Amnesty inawashutumu Hamas pia kwa madai ya kupanigia haki na uhuru kwa wapelestina wakati wao wamekuwa hawafanyi mambo yanayofanana na yale wanayoyasema.
Shirika la Amnesty limeitaka Hamas kushirikiana na Tume ya uchunguzi ya kimataifa inayochunguza ukiukwaji huo wa haki za binadamu na kuwafikisha wote waliohusika kwenye mkono wa sheria.

No comments:

Post a Comment