Wednesday, 27 May 2015

AUSTRALIA YAIPIGA ‘JEKI’ VETA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLQkLgva6gN7_Rf1TlGjTVNtocv1Uk-3WjFoTOAK9rO357RfX2O4mKiOP_K4poj68Ay1Vzb8M35dyoP8uWYaP9cmMJJbvYPQ7QRwO-8M6ft8zvymQApnS7wg0PdU8CBnHBInTBHcGc4QZb/s1600/IMG_2564.JPG

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)imeanzisha mfumo wa mafunzo stadi katika sekta ya madini na gesi ambao utasaidia watu wanaohitimu katika mafunzo hayo duniani.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjhf8U8NtoxNRMkZ4HYoanUftOQ-qdgMIfFQHyGstLcTqxwHVsX9XeIqoTs6u0y7cxWzFr4oGavJPrlEvtkyzrUzidHohj4iQ6ga8WP7v_lcdJaCJY9Hh0Ear8VsiLK5SWBPaKmAh_O-aSr/s1600/IMG_2585.JPG


Hayo ameyasema leo Mkurugenzi Mkuu wa VETA,Mhandisi Zebadiah Moshi wakati wakisaini makubaliano na serikali ya Australia kuptia shirika la Idara ya Mambo ya Nje na Biashara (DFAT)iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi61AJKYUhJuNq3Ettgq-APqwEGhg0szs0ozwLRSz33J1lAn9irh2rMIIi6x4Q37f7Bxn0ZqSWrQJcCqlGebjNlAwHokPGrbhiwOme3_1Ej2Mi41jgJatsrpCoz8xp5NbyQ8sMBFqjdTkFE/s1600/IMG_2495.JPG
Amesema katika makubaliano hayo,Serikali ya Australia imekubali kutoa Sh.milioni 330  kwa ajili mfumo huo ambao utatengenezwa na wataalam wa nchi hiyo.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3IWyzwRvbpW2i91FF_cj1UwUjYS7WqE9_y7BKDApESmb01LGDNCp53aodLufOYFeld-SgisElp5ViZaR2j4mz9cYVFDXfWoGKCDqPfQFBgNKB7nnEsy6zBp-qOmN9MZy7-y4orO3SesO0/s1600/IMG_2531.JPG


Mhandisi Moshi amesema manufaa ya mfumo huo kwa VETA kuimarisha ushirikiano na viwanda au waajiri mbalimbali, kulenga kutoa mafunzo ambayo yanaendana na mahitaji ya soko la ajira,uboreshaji wa viwango vya mafunzo yanayotolewa na viwanda,kuipunguzia mzigo serikali katika kuilea VETA kwa kuchangia gharama za mafunzo kwa njia ya vifaa au kutoa wataalam wa kufundisha.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgt0XjypFeIYB8E66xnb4vE61_nXQuWI6iUlgED2ve9biLPKoqfhVdEJXRWkEKP7dyiBpT8m8wJh3ltRf4UDQEyiGswPocNPFyVXt5x45eM-lJDTizfp3EmVVwwEQp4vkGrhjBhOkzCc3iL/s1600/IMG_2602.JPG


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba akizungumza na waandishi habari katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment