Sunday, 24 May 2015

ANASWA NA SILAHA YA KIVITA

Na Gurian  Adolf
Sumbawanga
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia mkazi wa kijiji cha  Mazigo Tarafa ya Inyonga  Wilaya ya Mlele mkoani humo kwa tuhuma za kumkamata na  silaha ya kivita aina ya AK 47  pamoja na Gobore moja.
Mtuhumiwa huyo aliyekamatwa ametajwa kuwa ni  Emanuel  Herman (KAMTUPE) (36) ambae ni mkazi wa Kijiji cha Masigo Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoani  humo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema kuwa  tukio la kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na silaha hizo mbili lilitokea mei 22 majira ya  saa nane usiku  katika  Kijiji hicho cha Masigo.
Kidavashari alisema  mtuhumiwa huyo alikamatwa kufuatia taarifa kutoka kwa raia wema walizozitoa kwa askari wa wanyama pori kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akimiliki  silaha kinyume cha sheria na amekuwa akizitumia kwa uwindaji haramu.
Baada ya taarifa hizo  kuwafikia askari wa wanyama pori  walianza msako wa kumsaka mtuhumiwa huku wakiwa wanaongozwa na Afisa wa wanyama pori  Cedrick  Mashauri.
 Kidavashari alieleza  katika  msako wa askari  wa wanyama poli  hao walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa  Emanuel  Herman(KAMTUPE) akiwa  na bunduki mbili  moja aina ya   AK 47   na  nyingine  aina ya Gobore.
 Alisema mtuhumiwa alikuwa akimiliki  bunduki hizo  kinyume cha sheria na  alikuwa akizitumia katika ujangiri kwenye uwindaji haramu katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kwenye mapori ya akiba.
Mtuhumiwa bado anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi na anatarajiwa kufikiwa mahakamani mara baada ya uchunguzi utakapo kuwa umekamilika.
 Hivi karibuni Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi  waliweza kufanya doria na kufanikiwa kuwakamata watu watatu wakiwa na vipande vitatu vya meno ya Tembo  yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 11 ambayo walikuwa wakitaka kuyasafirisha kutoka kwenye Makazi ya  Katumba Wilaya ya Mlele  kuyapeleka  Mkoa wa Tabora
MWISHO

WANASIASA RUKWA WAONYWA

Na Gurian  Adolf
Sumbawanga

SERIKALI ya mkoa wa Rukwa imewaonya baadhi ya wananchi na wanasiasa kutodhubutu kuwaingiza watu nchini kinyume na sheria ili wajiandikishe katika daftari la kudumu la wapigakura kwa lengo wawapigie kura wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Onyo hilo alilitoa jana na mkuu wa mkoa wa Rukwa Stella Manyanya wakati Akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa kuanza uandikishaji katika daftari la kudumu la wapigakura kazi inayoanza leo  Mei  24.

Alisema kuwa wapo baadhi ya wanasiasa ambao wanaweza kushawishika kuwaingiza nchini kinyume na sheria na kujiandikisha katika daftari la wapigakura ili nao wajewashiri katika  uchaguzi mkuu.

‘’mkoa wetu upo mpakani…tunapakana na nchi za Zambia na Congo, hivyo basi ni kosa kisheria kuwaingiza watu nchini kinyume cha sheria pia vivyo hivyo ni kosa kisheria kwa mtu ambaye sio raia kujiandikisha katika daftari la kudumu hivyo nawaasa wananchi wajiepushe kuwaingiza watu nchini kinyume cha sheria’’…….alisema.

Alisema kuwa kutokana na zoezi hilo kuwa linaanza leo hivyo basi nivizuri kwa wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha ili wapate fursa ya kuchagua viongozi wao katika uchaguzi mkuu.

Manyanya alisema kuwa wanasiasa wawe makini na mchakato huo kuepusha hisia zao za kisiasa kwani wasipokuwa makini wanaweza kusababisha zoezi hilo likaingia dosari kwani huu ni wakati wa kutazama maslahi mapana ya taifa.

Hata hivyo alitoa wito kwa waandikisha katika zoezi hilo kuwa makini na kufuata sheria na taratibu walizofundishwa ili kutosababisha mkanganyiko wowote ili zoezi hilo lifanyike kwa umakini na kwa muda unaotarajiwa.

Mwisho

WANANDOA WACHINJWA KAMA KUKU

Na Gurian  Adolf
Sumbawanga 
WATU  wawili ambao ni mke na mume  wakazi wa Kitongoji cha Makambo  Kata ya Itenka Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wameuwawa kikatili kwa kuchinjwa hadi kutenganishwa kichwa  na kiwiliwili  wakati wakiwa wamelele ndani ya nyumba yao.
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  aliwataja wanandoa hao  kuwa ni  Seth Mwakalimbwa (65) na Yakoba  Kalulu(48)  wakazi wa kitongoji hicho ambao waliuawa na watu wasiofahamika.
Kidavashari aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo la mauwaji ya kikatili lilitokea Mei 21 majira ya  usiku  nyumbani kwa wanandoa hao ambao waliuwawa kwa kuchinjwa na kisha miiliyao kuachwa kitandani.
Alisema  marehemu  hao wakati wa uhai wao walikuwa  wakiishi  kwenye nyumba  yao  huku  wakiwa p eke yao  pasipo kuwa na  watu wengine kwenye nyumba hiyo waliishi kwa muda mrefu.
Siku mbili baadaye  balozi wa eneo hilo aitwaye  Wilbroad Mahenge  ambae  ni jirani wa marehemu  hao  aliingiwa na mashaka  baada ya kutowaona  wanandoa hao wawili kwa kipindi cha siku mbili mfululizo.
 Kamanda Kidavashari alieleza  balozi huyo  kutokana na kutowaona  wanandoa hao  aliamua  kufika  katika makazi yao  kwalengo la kuwasahabi  na alipofika hapo  alikuta  milango ya nyumba yao   iko wazi hali iliyosababisha apate mashaka.
 Alisema alijaribu kuwaita kwa majina yao lakini hakuna  aliyeweza kuitika   na aliamua  kuingia ndani  ya nyumba hiyo  ndipo  aliwakuta wakiwa  wamelazwa kitandani  huku   wakiwa wamefariki dunia kwa kuchinjwa shingo zao na kutenganishwa kiwiliwili na kichwa.
Baada ya kuona hivyo balozi  Wilbroad  alitoka nje na kisha kwenda kutowa taarifa kwenye uwongozi wa Serikali ya Kitongoji ambao na wao walitoa taatifa kwa jeshi la polisi ambao walifika kwenye eneo la tukio baada ya muda mfupi.
Kamanda Kidavashari alisema  chanzo cha  tukio la mauwaji hayo linahusishwa  na imani  za  kishirikina  na mpaka sasa  hakuna mtu  wala watu  waliokamatwa  kuhusika na tukio hilo.
 Aidha  jeshi la polisi kwa kushirikiana  na uongozi  na wanakijiji  wa Makambo  wanaendelea  na msako  ili  kuwabaini  watu  waliohusika  katika mauwaji ya wanandoa hao.
MWISHO

Monday, 4 August 2014

walimu Rukwawapewa siku 14 waanze kutoa chakula shuleni

Na Gurian Adolf
Sumbawanga.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa ametoa siku 14 kwa watendaji wa vijiji kuhakikisha shule zilizopo katika vijiji yao zinatoa chakula kwa wanafunzi atakaye shindwa awekwe ndani kwa siku saba.

Agizo hilo lilitolewa jana na kaimu mkurugenzi Chrispin Mlwanda katika mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kaengesa wilayani humo kwa lengo la kukaugua utekelezaji wa sera ya matokeo makubwa sasa (BRN).

Alisema kuwa baadhi ya watendaji wa vijiji wamekuwa ni kikwazo cha utekelezaji mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu.

Alisema kutokana na hali hiyo sasa ni wakati wa kuanza kuwawajibisha watendaji wa vijiji kwani kulegalega kwao kumekuwa ni kikwazo cha maendeleo.

"natoa siku 14 kwa watendaji wa vijiji wote kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata chakula, kwa mtendaji atakayeshindwa akamatwe na kuwekwa ndani kwa siku saba ili iwe fundisho"...alisema

kaimu huyo mkurugenzi alisema kuwa changamoto nyingi katika shule za msingi katika halmashauri hiyo zinaweza kutatuliwa lakini tatizo ni viongozi wa serikali wamekuwa hawawajibiki kutekeleza majukumu yao.

Kwaupande wake Afisa elimu shule za sekondari wilayani humo Emiliana Fungo alisema kuwa wazazi wanawajibu wa kuhakikisha wanatatua changamoto kaika shule ambazo wanasoma watoto wao ili waweze kupata matokeo bora.

Mwisho.

Friday, 25 July 2014

Wazazi Sumbawanga mkoani Rukwa waomba kucharazwa mboko na walimu

Na Gurian  Adolf
Sumbawanga.

Baadhi ya wazazi katika kata ya Lusaka wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wamemuomba kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Chrispine Mrwanda kupeleka ombi lao kwenye baraza la madiwani ili lipitishe kuwa sheria ambayo itawapa uwezo walimu wa kuwacharaza viboko baadhi ya wazazi wasiowatimizia mahitaji ya elimu watoto wao.

Ombi hilo walilitoa jana katika viwanja vya serikali ya kijiji hicho ambapo Idara ya elimu halmashauri hiyo ilikuwa ikifanya ziara yenye lengo kuboresha ufaulu katika shule za msingi na sekondari ikiwa ni utekelezaji wa sera ya matokeo makubwa sasa (BRN) katika halmashauri hiyo.

Mmoja wa wazazi hao Datus Seleman alimuomba kaimu mkurugenzi huyo kupokea ombi kutoka kwa wazazi wa kata hiyo kuliomba baraza la madiwani kuanziasha sheria ndogo itakayo waruhusu walimu kuanza kuwachapa viboko wazazi wote ambao hawawatimizii watoto wao mahitaji ya elimu.

Alisema kuwa wapo baadhi ya wazazi wamekuwa hawajali kuhusu watoto wao kama wanakwenda hata shuleni ikiwa ni pamoja na kuwanunulia sare za shule, madaftari na michango mbalimbali kitu ambacho kinapaswa kuwa ni kosa la kisheria.

Naye bi Maria Maivune alisema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakitumia pesa zao kwa kunywa pombe na kuoa wanawake wengi na hivyo kushindwa kuwahudumia watoto wao.

"nadhani kama wazazi hao wangekuwa wanacharazwa viboko na walimu labda wanaweza kubadirika kutokana na aibu ya kuchapwa huenda wakaanza kuwajali watoto wao".....alisema.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi Mlwanda alisema kuwa halmashauri itakachopaswa kufanya ni kuwabana wazazi hao ili waweze kutimiza wajibu wao wakuwapa mahitaji wanafunzui hao ili malengo ya BRN yaweze kutekelezeka katika Halmashauri hiyo.

Mwisho.

Mvuta bangi anusurika kwenda jela miaka miwili

Na Gurian Adolf
Sumbawanga

MUUZA JI wa dawa  za kulevya  aina ya bangi , Ferdinand Makundi (40)
amenusurika  kwenda jela miaka  miwili jela  baada kulipa
faini  ya Sh 100,000- kwa kosa la kukutwa  na  kilo mbili  za bangi.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama  ya Wilaya  ya Nkasi , mkoani Rukwa ,
Ramadhani Rugemalira  alimuhukumu  mshtakiwa huyo  ambaye ni mkazi wa
kijiji cha Mkole  wilayani  humo  kutumikia miaka miwili jela  au
kulipa  faini ya Sh 100,000-  baada ya kukiri kosa lake  mbele ya
mahakama hiyo .

Hata  hivyo mahakama  hiyo ilimwachia  mshtakiwa  huyo  baada ya
kulipa faini  hiyo  mahamani hapo .

Mshtakiwa  huyo  alikiri  kosa lake  hilo  baada ya Mwendesha Mashtaka
, Mkaguzi Msaidizi , Hamimu Gwelo  kumsomea  jana makosa  yake  ya
awali .

Kwa mujibu  wa Gwelo , mshtakiwa huyo  ni mzoefu  kwa  sababu aliwahi
awali  kutiwa  hatiani  na mahakama  hiyo  kwa kosa  la  kukutwa na
dawa  ya kulevya aina ya bangi  pia aliweza  kulipa faini na kuachiwa
hivyo aliiomba  mahakama impatie  adhabu kali  kwa kuwa bado
hajajifunza .

Hati  za mashtaka  mahakamani hapo  zinaonesha kuwa mshtakiwa huyo
alitenda  kosa hilo Mei , 14 mwaka  huu saa saba mchana  akiwa
nyumbani kwake  kijijini Mkole .
Alipotakiwa  kujitetea , mshtakiwa  aliiomba mahakama  hiyo impunguzie
adhabu  kwa kuwa  ana watoto  kumi na  mke  wanaomtegemea .
Mwisho

Thursday, 12 June 2014

WATUMISHI WA AFYA WATAKIWA KUHESHIMU MAADILI YA KAZI.

Na Gurian Adolf
Sumbawanga

Serikali mkoani Rukwa imewaagiza watumishi wa idara ya afya mkoani humo kuzingatia maadili ya kazi hasa kwa kutovujisha siri za wateja wao pindi wanapofika kupata huduma.

Agizo hilo limetolewa na mwakilishi wa mkuu wa mkoa huo Iddy Kimanta ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Nkasi wakati akizindua kampeni za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto.

Alisema kuwa kitendo cha baadhi ya watendaji wa afya kutokuwa na siri hususani kwa watu wanaopima virusi vya ukimwi kumekuwa kukisababisha watu wengi kuacha kujitokeza kupima.

"baadhi yenu mmekuwa mkitoa siri za wateja wenu maana mtu anapima asubuhi kufikia jioni taarifa zote za vipimo vyako unavikuta mtaani" alisema.

Alisema kuwa kitendo hicho ni ukoseefu wa maadili ya kazi na kinadhoofisha kampeni mbalimbali zinazohusu masuala ya kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi.

Kwaupande wake mganga mkuu wa mkoa wa Rukwa John Gurisha alisema kuwa kasi ya maambukizi mapya ya VVU inazidi kuongezeka ambapo hivi sasa imefikia kiwango cha asilimia 6.2 huku kiwango cha kitaifa ni asilimia 4.5

mwisho