Na Gurian Adolf
Sumbawanga
WATU wawili ambao ni mke na mume wakazi wa Kitongoji cha Makambo Kata ya Itenka Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya
Mlele Mkoa wa Katavi wameuwawa kikatili kwa kuchinjwa hadi kutenganishwa kichwa na kiwiliwili wakati wakiwa wamelele ndani ya nyumba yao.
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari aliwataja wanandoa hao kuwa ni Seth
Mwakalimbwa (65) na Yakoba Kalulu(48) wakazi wa kitongoji hicho ambao waliuawa na watu wasiofahamika.
Kidavashari aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio
hilo la mauwaji ya kikatili lilitokea Mei 21 majira ya usiku
nyumbani kwa wanandoa hao ambao waliuwawa kwa kuchinjwa na kisha miiliyao kuachwa kitandani.
Alisema marehemu
hao wakati wa uhai wao
walikuwa wakiishi kwenye nyumba yao
huku wakiwa p eke yao pasipo kuwa na watu wengine kwenye nyumba hiyo waliishi kwa
muda mrefu.
Siku mbili baadaye balozi wa eneo hilo aitwaye Wilbroad Mahenge ambae
ni jirani wa marehemu hao aliingiwa na mashaka baada ya kutowaona wanandoa hao wawili kwa kipindi cha siku
mbili mfululizo.
Kamanda Kidavashari
alieleza balozi huyo kutokana na kutowaona wanandoa hao
aliamua kufika katika makazi yao kwalengo la kuwasahabi na alipofika hapo alikuta milango ya nyumba yao iko wazi hali iliyosababisha apate mashaka.
Alisema alijaribu
kuwaita kwa majina yao lakini hakuna
aliyeweza kuitika na
aliamua kuingia ndani ya nyumba hiyo ndipo
aliwakuta wakiwa wamelazwa
kitandani huku wakiwa wamefariki dunia kwa kuchinjwa shingo
zao na kutenganishwa kiwiliwili na kichwa.
Baada ya kuona hivyo balozi Wilbroad alitoka nje na kisha kwenda kutowa taarifa
kwenye uwongozi wa Serikali ya Kitongoji ambao na wao walitoa taatifa kwa
jeshi la polisi ambao walifika kwenye eneo la tukio baada ya muda mfupi.
Kamanda Kidavashari alisema
chanzo cha tukio la mauwaji hayo linahusishwa na imani
za kishirikina na mpaka sasa
hakuna mtu wala watu waliokamatwa
kuhusika na tukio hilo.
Aidha jeshi la polisi kwa kushirikiana na uongozi
na wanakijiji wa Makambo
wanaendelea na msako ili kuwabaini
watu waliohusika
katika mauwaji ya wanandoa hao.
MWISHO
No comments:
Post a Comment