Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MUUZA JI wa dawa za kulevya aina ya bangi , Ferdinand Makundi (40)
amenusurika kwenda jela miaka miwili jela baada kulipa
faini ya Sh 100,000- kwa kosa la kukutwa na kilo mbili za bangi.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nkasi , mkoani Rukwa ,
Ramadhani Rugemalira alimuhukumu mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa
kijiji cha Mkole wilayani humo kutumikia miaka miwili jela au
kulipa faini ya Sh 100,000- baada ya kukiri kosa lake mbele ya
mahakama hiyo .
Hata hivyo mahakama hiyo ilimwachia mshtakiwa huyo baada ya
kulipa faini hiyo mahamani hapo .
Mshtakiwa huyo alikiri kosa lake hilo baada ya Mwendesha Mashtaka
, Mkaguzi Msaidizi , Hamimu Gwelo kumsomea jana makosa yake ya
awali .
Kwa mujibu wa Gwelo , mshtakiwa huyo ni mzoefu kwa sababu aliwahi
awali kutiwa hatiani na mahakama hiyo kwa kosa la kukutwa na
dawa ya kulevya aina ya bangi pia aliweza kulipa faini na kuachiwa
hivyo aliiomba mahakama impatie adhabu kali kwa kuwa bado
hajajifunza .
Hati za mashtaka mahakamani hapo zinaonesha kuwa mshtakiwa huyo
alitenda kosa hilo Mei , 14 mwaka huu saa saba mchana akiwa
nyumbani kwake kijijini Mkole .
Alipotakiwa kujitetea , mshtakiwa aliiomba mahakama hiyo impunguzie
adhabu kwa kuwa ana watoto kumi na mke wanaomtegemea .
Mwisho
No comments:
Post a Comment