Na Gurian Adolf
Sumbawanga
WATOTO watatu wanasadikika kufa maji na watu wengine 11 wameokolewa baada ya boti walilokuwa wanasafiria kuzama Katika ziwa Tanganyika.
Tukio hilo likitokea Septemba 13 majira ya saa 11:00 Jioni katika Kijiji cha Kalila kata ya Kabwe, tarafa ya Kirando, wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Rukwa George Kyando alisema kuwa boti hilo ambalo halina jina na mmiliki wake hajajulikana lilikuwalikitokea kirando kwenda Kijiji cha Kyala mkoani Kigoma ilipinduka na kuzama ndani ya Ziwa Tangnyika na kusababisha kifo cha mtoto aliyejulikana kwa jina la Yakin Said(miezi mwili).
Alisema kuwa katika boti hilo kulikuwa na watu 14 ambao kati yao walikuwa ni wafanyakazi wawili, abiria 11 ambao wote waliokolewa naabiria wenzao wanaofahamu kuogelea.
Baada ya ajali hiyo wafanyakazi hao wawili waliogelea na kutoroka hukuwakiwaacha abiria wao ndani ya maji bila msaada kanakwamba waliwatosa majini.
Kamanda Kyando alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hali ya hewa kuwa mbaya ambapo kulikuwa na upepo mkali ziwani uliopelekea mawimbi makali ambapo upepo huo ulivuma na hata kuezua nyumba za baadhi ya wakazi waliojenga ufukweni mwa Ziwa hilo eneo ambalo boti hilo lilizama.
Banda ya kuokolewa walifanikiwa kuutafuta mwili wa mtoto aliyefariki na kukabidhiwa kwa wazazi wake ambao nao walikuwa ni abiria kwa ajili ya mazishi huku watoto wengine bado wanatafutwa.
Hata hivyo kamanda huyo wa polisi alitoa wito kwa abilia kutosafiri majini pindi wanapoona kunaupepo mkali na dhoruba ili waweze kuwa salama Katika safari zao.
Mwisho
No comments:
Post a Comment