Na Gurian Adolf
Sumbawanga
SERIKALI ya
mkoa wa Rukwa imewaonya baadhi ya wananchi na wanasiasa kutodhubutu kuwaingiza
watu nchini kinyume na sheria ili wajiandikishe katika daftari la kudumu la
wapigakura kwa lengo wawapigie kura wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
Onyo hilo
alilitoa jana na mkuu wa mkoa wa Rukwa Stella Manyanya wakati Akizungumza na
vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa kuanza uandikishaji katika daftari
la kudumu la wapigakura kazi inayoanza leo
Mei 24.
Alisema kuwa
wapo baadhi ya wanasiasa ambao wanaweza kushawishika kuwaingiza nchini kinyume
na sheria na kujiandikisha katika daftari la wapigakura ili nao wajewashiri
katika uchaguzi mkuu.
‘’mkoa wetu
upo mpakani…tunapakana na nchi za Zambia na Congo, hivyo basi ni kosa kisheria
kuwaingiza watu nchini kinyume cha sheria pia vivyo hivyo ni kosa kisheria kwa
mtu ambaye sio raia kujiandikisha katika daftari la kudumu hivyo nawaasa
wananchi wajiepushe kuwaingiza watu nchini kinyume cha sheria’’…….alisema.
Alisema kuwa
kutokana na zoezi hilo kuwa linaanza leo hivyo basi nivizuri kwa wakazi wa mkoa
huo kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha ili wapate fursa ya kuchagua viongozi
wao katika uchaguzi mkuu.
Manyanya alisema
kuwa wanasiasa wawe makini na mchakato huo kuepusha hisia zao za kisiasa kwani
wasipokuwa makini wanaweza kusababisha zoezi hilo likaingia dosari kwani huu ni
wakati wa kutazama maslahi mapana ya taifa.
Hata hivyo
alitoa wito kwa waandikisha katika zoezi hilo kuwa makini na kufuata sheria na
taratibu walizofundishwa ili kutosababisha mkanganyiko wowote ili zoezi hilo
lifanyike kwa umakini na kwa muda unaotarajiwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment