Na Gurian Adolf
Sumbawanga
Jeshi la Polisi
Mkoa wa Katavi linamshikilia mkazi wa kijiji cha Mazigo Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele mkoani humo kwa tuhuma za
kumkamata na silaha ya kivita
aina ya AK 47 pamoja na Gobore moja.
Mtuhumiwa huyo
aliyekamatwa ametajwa kuwa ni
Emanuel Herman (KAMTUPE) (36) ambae
ni mkazi wa Kijiji cha Masigo Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoani humo.
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema kuwa tukio la kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na
silaha hizo mbili lilitokea mei 22 majira ya
saa nane usiku katika Kijiji hicho cha Masigo.
Kidavashari
alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa
kufuatia taarifa kutoka kwa raia wema walizozitoa kwa askari wa wanyama
pori kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akimiliki
silaha kinyume cha sheria na amekuwa akizitumia kwa uwindaji haramu.
Baada ya taarifa
hizo kuwafikia askari wa wanyama
pori walianza msako wa kumsaka mtuhumiwa
huku wakiwa wanaongozwa na Afisa wa wanyama pori Cedrick
Mashauri.
Kidavashari alieleza katika
msako wa askari wa wanyama
poli hao walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Emanuel Herman(KAMTUPE) akiwa na bunduki mbili
moja aina ya AK 47 na
nyingine aina ya Gobore.
Alisema mtuhumiwa alikuwa akimiliki bunduki hizo
kinyume cha sheria na alikuwa
akizitumia katika ujangiri kwenye uwindaji haramu
katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kwenye mapori ya akiba.
Mtuhumiwa bado
anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi na anatarajiwa kufikiwa mahakamani
mara baada ya uchunguzi utakapo kuwa umekamilika.
Hivi karibuni Askari wa Hifadhi ya Taifa ya
Katavi waliweza kufanya doria na
kufanikiwa kuwakamata watu watatu wakiwa na vipande vitatu vya meno ya
Tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 11 ambayo walikuwa wakitaka kuyasafirisha kutoka kwenye Makazi ya Katumba Wilaya ya Mlele kuyapeleka
Mkoa wa Tabora
MWISHO
No comments:
Post a Comment