Na Gurian Adolf
Sumbawanga
Serikali mkoani Rukwa imewaagiza watumishi wa idara ya afya mkoani humo
kuzingatia maadili ya kazi hasa kwa kutovujisha siri za wateja wao pindi
wanapofika kupata huduma.
Agizo hilo limetolewa na mwakilishi wa mkuu wa mkoa huo Iddy Kimanta
ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Nkasi wakati akizindua kampeni za kuzuia
maambukizi ya VVU kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto.
Alisema kuwa kitendo cha baadhi ya watendaji wa afya kutokuwa na siri
hususani kwa watu wanaopima virusi vya ukimwi kumekuwa kukisababisha
watu wengi kuacha kujitokeza kupima.
"baadhi yenu mmekuwa mkitoa siri za wateja wenu maana mtu anapima
asubuhi kufikia jioni taarifa zote za vipimo vyako unavikuta mtaani"
alisema.
Alisema kuwa kitendo hicho ni ukoseefu wa maadili ya kazi na
kinadhoofisha kampeni mbalimbali zinazohusu masuala ya kukabiliana na
ugonjwa wa ukimwi.
Kwaupande wake mganga mkuu wa mkoa wa Rukwa John Gurisha alisema kuwa
kasi ya maambukizi mapya ya VVU inazidi kuongezeka ambapo hivi sasa
imefikia kiwango cha asilimia 6.2 huku kiwango cha kitaifa ni asilimia 4.5
mwisho
No comments:
Post a Comment