Na Gurian Adolf
Sumbawanga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa ametoa
siku 14 kwa watendaji wa vijiji kuhakikisha shule zilizopo katika vijiji
yao zinatoa chakula kwa wanafunzi atakaye shindwa awekwe ndani kwa siku
saba.
Agizo hilo lilitolewa jana na kaimu mkurugenzi Chrispin Mlwanda katika
mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kaengesa
wilayani humo kwa lengo la kukaugua utekelezaji wa sera ya matokeo
makubwa sasa (BRN).
Alisema kuwa baadhi ya watendaji wa vijiji wamekuwa ni kikwazo cha utekelezaji mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu.
Alisema kutokana na hali hiyo sasa ni wakati wa kuanza kuwawajibisha
watendaji wa vijiji kwani kulegalega kwao kumekuwa ni kikwazo cha
maendeleo.
"natoa siku 14 kwa watendaji wa vijiji wote kuhakikisha wanafunzi wa
shule za msingi wanapata chakula, kwa mtendaji atakayeshindwa akamatwe
na kuwekwa ndani kwa siku saba ili iwe fundisho"...alisema
kaimu huyo mkurugenzi alisema kuwa changamoto nyingi katika shule za
msingi katika halmashauri hiyo zinaweza kutatuliwa lakini tatizo ni
viongozi wa serikali wamekuwa hawawajibiki kutekeleza majukumu yao.
Kwaupande wake Afisa elimu shule za sekondari wilayani humo Emiliana
Fungo alisema kuwa wazazi wanawajibu wa kuhakikisha wanatatua changamoto
kaika shule ambazo wanasoma watoto wao ili waweze kupata matokeo bora.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment