Na Gurian Adolf
Kalambo
BAADHI
ya wavuvi mkoani Rukwa wameiomba serikali kuiokoa sekta hiyo kwa
kualika wawekezaji wakubwa ili wawekeze viwanda vya kusindika samaki
hali itakayo saidia kuwa na soko la uhakika la samaki mkoani sambamba na
kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda.
Wakizungumza na
gazeti hili walisema kuwa hivi sasa sekta ya uvuvi mkoani humo
inakabiliwa na hali ngumu baada ya serikali ya Zambia kupiga marufuku
uvuvi katika ziwa Tanganyika sambamba na kuingiza samaki kutoka katika
nchi jirani za Tanzania na Kongo kutokana na kipindupindu kwasababu
mkoani humo hakuna viwanda vya kusindika mazao ya ziwani.
Mmoja
wavuvi aliyepo katika kijiji cha Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa
Skeva Sinyangwe alisema kuwa hivi sasa sekta ya uvuvi imekabiliwa na
changamoto kutokana na kukosa soko la samaki ambapo kilogramu moja ya
samaki wamekuwa wakiuza chini ya shilingi 1,000 kutoka shilingi 5,000
waliyokuwa wakiuza hapo awali.
Alisema kuwa wavuvi wa
mkoani Rukwa walikuwa wakitegemea kuuza samaki wao nchini Zambia ambako
kuna makampuni yapatayo 12 ambapo yalikuwa yakinunua mpaka tani 1,200
ambao walikuwa wakiuza katika makasha ya mbao yenye uzito wa kilogramu
30 kwa shilingi 125,000 lakini tangu nchi hiyo ikabiliwe na kipindupindu
na kuzuia ununuaji wa samaki wababich bei imeporomoka.
Naye
Frances Simzosha mkazi wa Kasanga alisema kuwa kwakuwa hivi sasa
serikalin ya awamu ya tano imejikita katika uchumi wa viwanda ni vizuri
sasa ikafungua milango na kuwaalika wawekezaji wakubwa waweze kufika
mkoani Rukwa na kuwekeza katika viwanda vya kusindika samaki ambao
wanaonekana kukosa soka hivi sasa.
Alisema kuwa nia ya
serikali ya awamu ya tano ni kuona nchi inakwenda katika uchumi wa kati
kupitia sekta ya viwanda sambamba na kupatikana kwa ajira hali ambayo
fursa ipo kupitia sekta ya uvuvi katika ziwa hilo.
Simzosha
alisema kuwa sambamba na hayo pia nchi itapata fedha nyingi kutokana na
malipo ya kodi kitu ambacho raisi wa awamu ya tano John Magufuli
anataka kukiona na inawezekana iwapo yakiandaliwa mazingira mazuri.
Aliiomba
serikali kuitumia fursa hiyo vizuri ya kuanzisha viwanda ambayo
itawakwamua wavuvi katika lindi la umasikini,wananchi wanaohitaji ajira
sambamba na kuongeza pato la serikali litakalo iwezesha kupata fedha za
kuwahudumia wanchi wake.
Mwisho
No comments:
Post a Comment