Sumbawanga
MTOTO Hapness Churura(8) ambaye ni mlemavu wa viungo
hajawahi kutolewa nje kwa kipindi cha maisha yake yote tangu kuzaliwa
kwake kutokana na wazazi wake kuwa wanamficha ndani wakidai kuwa wanaona
aibu kwa jamii kutokana na kuwa na mtoto mlemavu.
Mtoto
huyo yupo katika Kijiji cha Chala C wilayani Nkasi mkoani Rukwa amekua
akifichwa ndani na wazazi wake na akipewa huduma zote za kibinadamu
humo ndani lakini hawakuweza kumtoa nje hata kuota jua kutokana na
kuona aibu familia hiyo kuwa na mtoto mremavu.
Mmoja
wa wakazi wa kijiji hicho Edwin Mselema akizungumza kwa njia ya simu na
mwandishi wa habari hii alisema kuwa kitendo walichokifanya wazazi hao
in kibaya na si cha kiungwana kinachopaswa kukemea na jamii nzima ya
kijiji hicho.
Alisema
kuwa kitendo hicho kimemnyima fursa nyingi mtoto huyo ikiwemo ni pamoja
na kusaidiwa na wakazi wa kijiji hicho, watu wengine wasamaria wema
pamoja na serikali kupitia mfuko wa maendeleo vijijini TASAF.
Mselema
alisema kuwa kitendo cha kumfungia ndani kimekiuka haki zake za msingi
kama kupata elimu, matibabu, kucheza na nyinginezo na hii inatokana na
baadhi ya watu kutokuwa na elimu dhidi ya watu Wenye ulemavu.
Alisema
mtoto Hapness amekuwa ni mremavu wa kulala kitandani kwa muda wote
tangu azaliwe kiasi kwamba amedhoofu afya yake kwa kutotoka nje kupata
jua pamoja na hewa na wakati mwingine kukosa mtu wa kumgeuza alipolala
pindi wanafamilia hiyo wanapokuwa wametoka kwenda kwenye shughuli zao.
"Sasa
wazazi wanahangaika kumlea kwa shida peke yao, wakati kama ingefahamika
kuwa wanamtoto mlemavu wangeweza kusaidiwa, hali ambayo inawazidishia
ugumu wa maisha na usumbufu wa kumficha mtoto huyo wakati si kosa
kuwa na mtoto mlemavu kwani ni mapenzi ya Mungu"... Alisema.
Alisema
kuwa bado serikali kupitia vyombo vya habari, pamoja na mashirika ya
ndani na nje yanawajibu wa kutoa elimu ili jamii iwachukulie watu Wenye
ulemavu kuwa ni binadamu wanaostahili haki zote hivyo kuwaficha ndani
ni makosa.
Mkazi huyo wa
kijiji cha Chala ambaye ni mdau wa masuala ya habari kijiji hapo alisema
kuwa jamii nayo inakua haijihusishi kujua kuhusu maisha ya watu
wengine kwani mama wa mtoto hiyo alibeba ujauzito lakini hawakujiuliza
hatma ya ujauzito ule ulikua ni ni ni kwani hawaoni mtoto wala hakukua
na taarifa kuwa mwanamke huyo amejifungua maiti, ama mtoto alifariki
baada ya kuzaliwa.
"
Najaribu kuvuta taswira hivi ingetokea mtoto huyo amefariki inamaana
wangeweka msiba, ama wangeenda kuzika usiku, mama wangeutupa mwili wake
porini maana kijijini watu walikuwa hawana taarifa za kuwepo kwa mtoto
hiyo mpaka Jana ambapo imefahamika sijui nini kingetokea iwapo mauti
yangemfika mtoto huyo" ... Alisema Maria Kasamya huku akiangua kilio
kwa uchungu.
Naye Coleta
Kachonta mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa huo ni ukatili wa haki ya
juu aliofanyiwa Hapness ambao inapaswa hatua za kisheria zichukuliwe kwa
wazazi wake ili wananchi wengine wajifunze kupitia tukio hilo ambalo
limesababisha mateso makubwa kwa takribani miaka 8 ya mtoto huyo tangu
kuzaliwa kwake.
Naye
Mwenyekiti wa kijiji hicho John Kapongwa akizungumza kwa njia ya simu
alisema kuwa hata yeye anashaa kuwepo kwa mtoto huyo katika kijiji
hicho kwani walikuwa hafahamu kabisa ila anashangaa na aliwashukuru
majirani waliosababisha kujulikana kuwepo kwa mtoto huyo.
Alisema
kuwa itabidi serikali ya kijiji ifanye kila liwezekanalo ili tabia
hiyo ikomeshwe katika kijiji hicho na kutafuta watu waweze kutoa elimu
ili jamii ibadilishe dhana potofu waliyokuwa nayo dhidi ya watu Wenye
ulemavu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment