Sumbawanga
KAIMU Mkuu wa shule ya Kanda Sekondari iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa amewaomba viongozi wa madhahebu ya dini kufanya maombi maalumu katika shule hiyo ili kuwaombea wanafunzi wanaougua ugonjwa wa ajabu wa kuanguka.
Akizungumzia na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni kaimu mkuu wa shule hiyo Mesko Mahenge alisema kuwa kumekuwepo kwa ugonjwa wa kupiga kelele kisha kuanguka kwa wanafunzi katika shule hiyo kwa muda mrefu hivis asa.
Alisema kuwa wanafunzi katika shule hiyo wamekuwa wakipatwa na ugonjwa huo tangu mwaka 2011 lakini hivi sasa ni wanafunzi wanne tu wa kike ndio wanasuombuliwa licha ya kuwa jitihada mbalimbali zimefanyika kuumaliza lakini bado hazijazaa Matunda.
Mwalimu Mahenge alisema kuwa alijitahidi kuwasiliana na wataalamu wa afya ambao walimueleza kuwa ni ugonjwa wa kisaikolojia,lakini pia amemua kuwashirikisha viongozi wa dini ili nao wa waombee wanafunzi hao huenda hali hiyo itakwisha.
Alisemabaadhi ya wanafunzi wanapokuwa wamepatwa na hali hiyo wanawapiga wenzao wanaokuwa wamewashika na wakati mwingine wanashika mawe nakuanza kuwatupia walimu na wanafunzi wenzao hali ambayo ni hatari kwani wanaweza hata kuwaumiza.
Hata hivyo mwandishi wa habari aliwashuhudia viongozi wa dini ya kiislamu wakiwa wamemaliza kufanya maombi shuleni hapo kwalengo la kuombea hali hiyo ya kuanguka wanafunzi iweze kuisha lakini pia mkuu huyo wa shule alisema kuwa viongozi wa madhehebu mbalimbali wataendelea kwenda kuwaombea kwakua tayari alikwisha ongea nao na wamekubali.
Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya wazazi ambao watoto wao wanasoma katika shule hiyo walisema kuwa wanafunzi hao wamekuwa wakipagawa na mapepo hivyo kufanya maombi shuleni hapo ni suala muhimu.
Mmoja wa wazazi aliyejitambulisha kwa jina la Alfred Kashamakula alisema kuwa kitendo cha kuwashirikisha viongozi wa dini wawaombee wanafunzi hao kitasaidia na kumaliza kabisa tatizo hilo.
"hayo yatakua ni mapepo kwakua mkuu wa shule ameamua kuwashirikisha viongozi wa dini wafanye maombi bila shaka muarobaini wa tatizo hilo umepatikana naamini hali hiyo haitaendelea tena"alisema Monica Kayuti.
Alisema kuwa hakuna sababu za kumsaka mchawi wa tatizo hilo kwani ni lakawaida kuwapata binadamu hata watu wazima huwa wanakabiliwa na hali kama hiyo isipokuwa watumie njia ya maombi litakwisha na wanafunzi wataendelea na masomo yao kama kawaida.
Mwisho
No comments:
Post a Comment