Na Walter Mguluchuma
Katavi
Zaidi ya shilingi bilioni 11 zimetengwa kwaajili ya kuboresha barabara katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.
fedha hizo ni mpango wa uboreshaji miundo mbinu ya miji yaani ULGSP uliopangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano ambapo miradi saba imepangwa kutekelezwa katika halmashauri 18 hapa nchini.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Enelia Lutungulu amebainisha hayo wakati wa mkutano wa wadau wa mpango kabambe wa Master plan ya miaka 20 ya Manispaa hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.
Alisema mpango wa uboreshaji wa miundo mbinu katika Halmashauri hiyo ulianza toka mwaka wa fedha wa 2013 na 2014 na utakamilika mwaka wa fedha wa 2017 na2018.
Kwamujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Manispaa hiyo ilikuwa na jumla ya wakazi 102,900 hivyo kupelekea kwenye mpango huo kupata mgao wa Dola za kimarekani 7,342,975, ambazo nisawa na shilingi za kitanzania 11,750,000,000 ambazo zitatumika kutekelezwa mpango huo kwa muda wa miaka mitano.
Lutungulu aliitaja miradi saba iliyopangwa kutekelezwa kwenye mradi huo kuwa ni usanifu wa miradi ya barabara na ujenzi wa soko la kisasa katika Kata ya Kazima, ujenzi wa Stendi ya mabasi ya kisasa katika eneo la Ilembo, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 7.7 Mpanda Mjini na uandaaji wa mpango kabambe wa Manispaa ya Mpanda na kujenga uwezo.
Mradi huo utakekelezwa na mtaalamu mshauri City Plan Consultancy T Limeted kwa gharama ya shilingi za kitanzania 283 600,000 Fedha ambazo zimetolewa na Manispaa ya Mpanda kupitia mpango wa utekelezaji wa miji unaofdhiliwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia.
Alifafanua kuwa mpango kabambe Master Plan wa Manispaa hiyo ulitangazwa kuanza mwaka 2010 lakini ulisimamishwa kutokana na kuongezeka kwa maeneo ya utawala hivyo mpango huo unatangazwa upya.
Iddy Mwerangi Afisa Mipango miji mshauri wa City Plan Consultancy T Limeted alisema kuwa ni lazima nguvu ziunganishwe za wadau mbalimbali wanaoweza kusaidia kupatikana kwa taarifa mbalimbali zitakazowezesha uaandaaji wa mpango Kabambe .
Alisisitiza kuwa swala hilo linahitaji kushirikisha wananchi kwani uzoefu unaonesha kuwa maeneo ambayo wananchi wamekuwa hawashirikishwi kumekuwa na migogoro.
Naye Makamu Meya wa Manispaa ya Mpanda John Matongo alisema swala hilo bila ushirikiano wa wananchi haliwezi kufanikiwa hivyo wao kama madiwani watahakikisha zoezi hilo la mpango Kabambe wa Master Plan linafanikiwa.
Kwaupande wake mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali mstaafu Raphael Muhuga alisema kuwa mji wa Mpanda unakuwa kwa hivyo ni vema maeneo ya mji huo yakawa yamewekwa kwenye mpango unaoeleka.
Alisema kuwa katika mpango huo wahakikishe pia wanatenga maeneo kwaajiri ya wakulima na wafugaji kwani kwa sasa yapo baadhi ya maeneo watu wanashindwa kulima kutokana na wafugaji kuvamia maeneo ya wakulima.
Aliongeza kusema kuwa nchi hii inaendeshwa kwa misingi ya sheria na hakuna mtu aliyejuu ya sheria hivyo kwa mtu yoyote ambaye ataamua kuishi kinyume na utaratibu wa matumizi bora ya ardhi yalivyo pangwa ajue kuwa hatua lazima zitachukuliwa dhidi yake.
Mwisho
No comments:
Post a Comment