Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MKOA wa Rukwa bado unakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo jumla ya vyumba 4,226 vinakitajika ili kumaliza tatizo hilo.
Akizungumza
hivi karibuni afisa elimu mkoa huo Nestory Mroka alisema kuwa mahitaji
hayo yamekuwa yakisababisha mkoa huo kutopiga hatua katika mafanikio ya
elimu.
Alisema
kuwa ili wanafunzi waweze kufanya vizuri katika masomo yao ni lazima
kuwe na miundombinu mizuri walimu wakutosha,vitabu pamoja na walimu
lakini kama kuna mapungufu kati ya hayo mambo hata ufaulu hauwezi kuwa
mzuri.
Mroka
alisema kuwa kutokana na changamoto hizo jitihada za makusudi
zinahitajika katika kulimaliza tatizo hilo pamoja na mengine ili kuweza
kuinua ufaulu wa wanufunzi katika shule za msingi pamoja na sekondari
ambapo mpaka sasa ufaulu katika kidato cha nne ni wastani wa daraja la
nne.
Afisa
elimu huyo alisema kuwa yeye binafsi amejitahidi kuhakikisha
anawasimamia walimu ili waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo ikiwamo ni
pamoja na kuwepo kazini kwa muda muafaka sambamba na kufundisha kwa
juhudi zote ili idara ya elimu iweze kuwa ya mfano wa kuigwa kwa kufanya
vizuri mkoani humo.
Kwaupande wake mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo aliziagiza halmashauri zote za mkoa huo kuhakikisha zikuja na mikakati ya kumaliza tatizo hilo pamoja na kwamba limeongezeka baada ya serikali ya awamu ya tano kuja na sera ya elimu bure.
Alisema
kuwa mafanikio yanakuja na changamoto zake lakini sio sababu ya
kulalamikia mafanio kilichopo ni kuzikabiri changamoto hizo kwani hivi
sasa kila mtoto mkoani humo awe wa tajiri ama masikini anauhakika wa
kupata elimu tofauti na miaka ya nyuma.
‘’ninakila
sababu ya kumpongeza muheshimiwa raisi John Magufuli kuamua serikali
yake kutoa elimu bure kwani hivi sasa kila mtoto wa mkoa huu anauhakika
wa kupata elimu kwakuwa inatolewa bila malipo hivyo ni wajibu wa mzazi
kuhakikisha mtoto anakwenda shule hata kama hana sare’’ alisema
Wangabo alisema kuwa huu ni wakati wa serikali,wazazi,wadau wa elimu na wadau wengine wa maendeleo kushirikiana
katika kumaliza changamoto hiyo kwani wakisubiri serikali peke yake
ifanye kazi hiyo mkoa utachelewa kupiga hatua katika elimu.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema kuwa hivi sasa serikali inajikita katika uchumi wa
viwanda lazima pia kuhakikisha kuwa elimu haibaki nyuma na mzizi wa
kufikia mafanikio hayo ni kuwekeza vizuri katika elimu kwani huko ndiko
watapatikana wataalamu watakao fanya kazi katika viwanda hivyo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment