Sumbawanga
BAADHI ya wakazi wa mkoani Rukwa wamemuomba rais John Magufuli kubadili msimamo na kuanza kuidhinisha wafungwa waliohukumiwa kunyongwa wanyongwe huenda hali hiyo itasababisha kupungua kwa mauaji holela yanayoendelea kutokea.
Ombi hilo limetolewa tolewa jana kwa nyakati tofauti baada ya kutokea mauaji ya telestina Silanda(45) mkazi wa kijiji cha China kata ya Kate wilayani Nkasi baada ya kuuawa kwa kuchinjwa na watu Wasiojulikana akiwanyumbani kwake.
mmoja wa wakazi wa mjini Sumbawanga aliyejitambulisha kwa jina la Frank Paschal alisema kuwa kutokana na kuwa adhabu ya kunyonga haijatekelezwa muda mrefu hapa nchini huenda ikawa ni sababu ya baadhi ya watu kufanya mauaji holale kwakua wanajua hata wakiua hawata nyongwa watakwenda kukaa gerezani kwa maisha yao yote.
Alisema kuwa kumbukumbu zinaonesha kuwa adhabu hiyo ilitekelezwa kwa rais wa awamu ya pili lakini marais waliofuata wamekuwa wakikwepa kuidhinisha watu waliohukumiwa kunyongwa,wanyongwe huenda ikawa ni sababu ya kuongezeka kwa mauaji holela ikiwemo ya vikongwe,albino na wanaotuhumiwa kwa ushirikina.
Paschal alisema kuwa hivi sasa watu hawana hofu tena ya kufanya mauaji hali ambayo inazidi kuota mizizi kutokana na kutotekelezwa hukumu ya kunyonga.
Naye Janeth Kapama mkazi wa wilaya ya Nkasi alisema kuwa kwakua sheria hiyo bado ipo na haijafutwa ni vizuri ikatekelezwa huenda itasaidia kuleta hofu katika jamii na kupunguza tabia ya baadhi ya watu kufanya mauaji holela.
"hivi vitendo vya viongozi wa nchi kutoridhia waliohukumiwa kunyongwa,wanyongwe kunachangia kuendelea kwa mauaji holela,kama hawataki basi sheria ifutwe kuliko kuwa nayo halafu haifanyiwi kazi" alisema
Alisema kumekuwa na kushamili kwa mauaji holela katika sehemu mbalimbali tena ukifuatilia unakutani sababu zisizo na msingi kama kuzushiwa ushirikina,tamaa ya mali na wivu wamaendeleo yote ni kutokana na kuwa wauaji hawanyongwi ndiyo sababu baadhi ya watu wamekuwa hawaogopi kuwaua wenzao.
Alimuomba rais Magufuli kusaini kutekelezwa kwa hukumu hiyo kwa nia njema ili kukomesha mauaji hayo tofauti na hivyo itakua ngumu kudhibiti mauaji holela kwani kitendi cha kuogopa kinasababisha baadhiya wa watu waendelee kuwaua wenzao kikatili.
"Tunajua rais wetu yupo makini katika kusimamia sheria za nchi kwani tumekuwa tukimuona ni msaada mkubwa kwa wanaoporwa viwanja,kubomoa wanaokiuka sheria za ujenzi na sheria nyingine nyinyi hivyo hapaswi kuogopa hii ya kuidhinisha wauaji kunyongwa kwani atakuwa anasimamia utawala wa sheria na si vinginevyo"alisema
Hata hivyo rais John Magufuli wakati akimuapisha jaji mkuu wa Tanzania alisema kuwa wasimpelekee mafaili ya watu walio hukumiwa kunyongwa kwani yeye binafsi hayupo tayari kuidhinisha watu hao wanyongwe.
Mwisho
No comments:
Post a Comment