Friday, 10 November 2017

Jela kwa utapeli

Na Gurian Adolf
Katavi
Mahakama ya  Hakimu  Mkazi Mkoa wa  Katavi imemuhukumu Kapele Mpundililwa(36)mkazi wa  Namanyere wilayani  Nkasi  mkoani Rukwa kutumikia kifungo cha  miaka  mitatu jela baada ya kumtia hatiani kwa utapeli na kujipatia fedha  kiasi cha zaidi ya  shilingi milioni 3.9
Mtuhumiwa huyo alijipatia fedha hizo baada ya  kuwalagai vijana 144 kuwa atawapatia ajira  katika Taasisi iIsiyo ya kiserikali ya APAPO.
Hukumu  hiyo ilitolewa jana  na hakimu mkazi wa  mahakama ya  mkoa wa Katavi  Odira  Amworo  baada ya kuridhika pasipo shaka yoyote na ushahidi uliotolewa.
Awali katika kesi  hiyo  mwendesha  mashta  mwanasheria wa  Serikali  wa mkoa wa  Katavi  Peter  Maiko  alidai  mahakamani  hapo kuwa   mshitakiwa alitenda  kosa hilo mei 23, 2013  wilayani Mpanda kwa  nyakati  tofauti.
 Mwanassheria  huyo  alidai kuwa  mshitakiwa  Kapeele  alifika wilayani Mpanda  na  kujitambulisha kuwa ni Mkurugenzi ya  Asiasi ya  Shirika la Umoja wa  Watu wa  Afrika  APAPO  na  alianza  kutangaza   nafasi mbalimbali za  ajira kwaajiri .
Miongoni mwa  njia alizotumia  kujipatia  fedha baada ya kutangaza ajira alimtaka kila aliyeomba atoe kiasi cha fedha iliapate kazi.
Mwanasheria   Peter  Maiko  aliieleza  mahakama hiyo kuwa ajira  kwa  ngazi ya mtaa  na  wilaya  kiwango cha ada ya  maombi ya  ajira  kilikuwa ni shilingi 17,000 na sifa  ilikuwa mwombaji lazima awe  na  elimu ya  darasa la  saba hadi kidato cha  nne na   ajira kwa  ngazi ya  mkoa  ada  ilikuwa ni shilingi 160,000   na  anaeomba  ajira  awe na  sifa ya kuanzia stashahada.
Alidai kuwa   mshitakiwa   huyo   katika  utapeli huo alifanikiwa kuwadanganya watu 144  ambao walilipa  ada za  maombi ya  ajira  hizo na kujipatia kiasi cha milioni 3,980,000 ambazo  zote ziliingizwa kwenye  akaunti  aliyokuwa  amewapatia na  shughuli hiyo ya  kutafuta  watu kwa  ajiri ya  ajira  alikuwa  akifanya  yeye  pamoja  na  wasaidizi wake  wanne ambao  walitoroka  baada ya  mkurugenzi wao  Kapeele kukamatwa mkoani   Kigoma  baada ya kuwa  ametoroka mkoani Katavi.
Akisoma hukumu  hiyo  hakimu  Amwolo  aliieleza  mahakama  kuwa  kutokana  na  mwenendo mzima wa kesi  hiyo na  ushahidi  uliotolewa   mahakamani  hapo na upande  wa mashitaka pasipo  shaka yoyote imemtia mshitakiwa  hatiani.
Hakimu  Amwolo  alieleza kuwa  miongoni  mwa  ushahidi  uliomtia   hatiani   mshitakiwa ni  hati za waliotapeliwa  ajira  walizolipia benki  ambazo  zilipelekwa  mahakamani hapo   huku  zikiwa  na majina ya waliotapeliwa na kiasi cha  fedha walizoingiza  kwenye  akaunti ya mshitakiwa
Alisema  mshitakiwa   amepatikana  na  hatia ya kifungu  cha   sheria   namba  302 cha  kanuni ya adhabu    sura ya 16   ya  marekebisho ya mwaka 2002 hivyo  Mahakama imemuhukumu   mshitakiwa kutumikia  jela kifungo cha  miaka  mitatu kuanzia  jana.
Mwisho

No comments:

Post a Comment