Friday, 10 November 2017

Viongozi wa dini waombwa kuuombea mkoa wa Rukwa

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
JESHI la polisi mkoani Rukwa limewaomba viongozi wa dini wazidi kumuomba Mungu ili lifanikiwe kumaliza vitendo vya mauaji ya nayotokana na imani za kishirikina mkoni humo.

Kamanda wa polisi mkoani humo George Kyando alitoa ombi hilo hivi karibuni kwa uongozi wa kanisa la Pool Of Siloam wakati akipokea msaada wa matairi Saba ya magari yaliyotolewa na kanisa hilo kwa lengo la kulisaidia jeshi hilo kukabiliana na uhaba wa vitendea kazi. 

Alisema kuwa miongoni mwa changamoto zinazoukabili mkoa wa Rukwa ni mauaji yanayotokana na imani za kishirikiana hivyo aliwaomba viongozi wa dini kuuombea mkoa huo ili mauaji hayo yaishe. 

Kamanda Kyando alisema jitihada zimefanyika za kutosha katika kukabiliana na kumaliza vitendo vya uhalifu lakini changamoto iliyopo ni mauaji yanayotokana na imani Za Kishirikiana.

Alisama jamii bila kumtegemea mwenyezi Mungu ni ngumu kuacha matendo maovu hivyo tasisi za dini zinajukumu hilo na iwapo wakiamua inawezekana kabisa binaadamu wanaishi kwa amani bila kutendeana matendo mabaya. 

Kwa upande wake kiongozi wa kanda ya Magaribi wa kanisa hilo mchungaji Wisdom Shangwe alisema kuwa wametoa Msaada wa matairi hayo yenye thamani ya shilingi 2,100,000 ili kulisaidia jeshi la katika kutekeleza majukumu yake. 

Alisema hivi sasa lengo  la kanisa hilo ni kusaidiana na serikali katika kuwasaidia vijana waweze kuachana na maovu pia waache kutumika na baadhi ya wanasiasa wa wasio na nia njema ambao wamekuwa wakiwatumia vijana kwa maslahi yao binafsi. 

Hata hivyo aliahidi kuendelea kuuombea mkoa hua pamoja na taifa kwa ujumla sambamba na viongozi wa serikali ili waendelee kumtumainia mwenyezi Mungu wakati wanapotekeleza majukumu yao.
Mwisho

No comments:

Post a Comment