Na Israel Mwaisaka
Nkasi
KIJANA aliyetambulika kwa jina la zakaria Katembo (30) mkazi wa kijiji cha Kakoma Kata ya Kipundu wilayani Nkasi mkoani Rukwa ameuawa kwa kupigwa mpini na watu wasiojulika na wanaodaiwa kuwa na hasira kali baada ya kukutwa akiiba mihogo shambani.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa kijiji cha Kakoma Patrick Mwami alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 4 za usiku baada ya wananchi wa kijiji hicho wanaodaiwa kuwa na hasira Kari kumvamia kijana huyo akiwa shambani alikokuwa akichimba mihogo na kumuua kwa kipigo.
Alisema kuwa wananchi baada ya kufanya mauaji hayo waliuacha mwili wa marehemu huyo katika shamba hilo na kuondoka na hawakubainika ni wakina nani waliofanya tukio hilo.
Naye diwani wa kata ya kipundu John Kapandila akizungumzia tukio hilo alisema kuwa baada ya tukio hilo aliutaka uongozi wa kijiji kutoa taarifa polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Pia aliitaka jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi badala yake wafuate sheria ili iweze kuchukua mkondo wake katika kuwaadhibu wahalifu.
Kwaupande wake mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo Said mtanda alisema kuwa watawasaka wale wote waliofanya mauaji hayo na kuwabaini ili sheria ichukue mkondo wake.
"tutawasaka watu waliofanya mauaji hayo na wenyetabia ya kuwaua binadamu kwasababu zozote zale kwani serikali haipotayari kuvumilia kuona mauaji yakitokea nawahakikishia lazima watuhiumiwa hao tuwafikishe kwenye vyombo vya sheria"alisema
Kamanda wa Polisi mkoani humo George Kyando alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watuhumiwa wa mauaji hayo ili wafikishwe kizimbani wakajibu tuhuma zitakazo wakabili.
Hata hivyo alionya tabia ya baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mikononi kwani kufanya hivyo ni makosa na lazima wanaofanya hivyo wachukuliwe hatua kali ili kukomesha mauaji holela.
mwisho
No comments:
Post a Comment