Na Israel Mwaisaka
Nkasi
SERIKALI wilayani Nkasi mkoani Rukwa imeliagiza jeshi la polisi wilayani humo kumkamata mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwai , Mashaka Aderson na wazazi wa watoto watatu waliokatiza masomo baada ya kupa ujauzito ili sheria ichukue mkondo wake.
Mkuu wa wilaya hiyo Said Mtanda alimuagiza mkuu wa Polisi Wilaya ya Nkasi ,(OCD) David Mtasya ili kumkamata mwalimu huyo mkuu pamoja na wazazi hao ambao wanaonesha wanakwamisha jitihada za serikali katika suala zima la kupambana na suala la wanafunzi kupata ujauzito.
Watoto hao watatu walimepata ujauzito wakiwa wanasoma darasa la Tano katikaShule ya Msingi Mwai iliyopo katika Kata ya Mtenga wilayani Nkasi katika mkoa wa Rukwa .
Mtanda alisema kuwa amelazimika kutoa agizo hilo kwa OCD baada ya kubainika kuwepo kwa mpango kati ya Mwalimu Mkuu ,Anderson na wazazi wa watoto hao kumaliza shauri hilo kwa usiri mkubwa pasipo kufikisha katika vyombo vya sheria.
Aidha mkuu huyo wa polisi wa wilaya ya tayari amekwisha tekeleza agizo hilo ambapo pia kasi alilieleza gazeti hili kuwa katika kukabiliana suala hilo amewakamata pia maofisa watendaji wa Kata wapatao sita wakituhumiwa kushirikiana na wazazi kumaliza kesi za mimba shuleni kwa siri.
Akizungumzia tatizo hilo Mtanda amesema kuwa katika wilaya ya Nkasi tatizo hilo ni kubwa ambapo sasa umekuwa kama mtindo ambapo watendaji wa kata , walimu wakuu wa shule na wazazi wanashirikiana kumaliza mashauri hayo kwa siri ili watoto hao waweze kuozeshwa kwa mahari ya fedha nyingi pamoja na ng'ombe.
“Kuanzia sasa kwa kuwa orodha ya watuhumiwa hao tunayo tutaanza mara moja katika vyombo vya habari" alisema

" kwa wale ambao wametoroka Serikali inatoa motisha ili wasakwe na kufikishwa katika vyombo vya dola …. Hatuwezi kamwe kuendelea na mtindo huu wa ovyo wa kuwavumilia watu wanaofanya vitendo vya namna hii “ alisisitiza.
Mtanda alibainisha hayo wakati alipokuwa akihutubia kikao maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo ambacho kilikuwa kikijadili hoja ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Mahesabu ya Serikali (CAG ) ambapo halmashauri hiyo imepata hati safi .
Mwisho

No comments:
Post a Comment