Sumbawanga
WAANDISHI
wa habari mkoani Rukwa wameshauriwa kujiunga na huduma za mfuko wa
Bima ya Afya ya Taifa ili waweze kujihakikishia kupata matibabu hata
wakati wakiwa wameugua na hawana fedha.
Ushauri
huo ulitolewa na Grory Mziray afisa kutoka ofisi za mfuko wa bima
ya afya ya mkoa wa Rukwa wakati akitoa mada katika kongamano la siku
ya Uhuru wa habari lililofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya
ya Sumbawanga mkoani humo.
Grory Mziray afisa kutoka ofisi za mfuko wa bima
ya afya ya mkoa wa Rukwa wakati akitoa mada katika kongamano la siku
ya Uhuru wa habari lililofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya
ya Sumbawanga mkoani humo.
Alisema
kuwa nivizuri sasa wanahabari wakajiunga na huduma za mfuko wa Bima
ya afya ya taifa kupitia fao la kikoa ambalo linatoa wigo kwa
wanachama walio katika vikundi vilivyo sajiliwa kwani chama chao
kimesajiliwa na kinatambulika kisheria.
Alisema
kuwa kwa kupitia fao hilo kila mchangiaji mmoja anapaswa kulipia
shilingi 76,800 na atapatiwa kitambulisho ambacho kitamuwezesha kutibiwa
katika vituo zaidi ya 6,900 vilivyopo nchi nzima.
Hata
hivyo katika kongamano hilo baadhi ya wadau wa habari walivilaumu
vyombo vya habari vya kitaifa kwakua vinazipa kipaumbele tu habari za
majiji makubwa kama Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika kongamano la wanahabari na wadau wa habari siku ya uhuru wa vyombo vya habari
Mmoja
wa wadau hao Anatory Sikulumbwe alisema kuwa miongoni mwa changamoto
ambazo zinawakumba wanahabari ni kuwa wengine
hawapendani maana aliyopo chumba cha habari yeye akipata mkataba
anaridhika na hajali kuhusu mwanahabari aliyepo mkoani ambaye ampelekea
habari kila siku.
Alisema
kuwa ikifika wakati wanahabari wakijitambua na kujaliana wataacha
kunyanyasika na kunyimwa haki zao kwani wanafanya kazi lakini wanakosa tija kutokana na kutokuwa na mikataba ya kazi.
Hata
hivyo aliwasihi wanahabari kutumia mitandao ya kijamii kwakua
wanahabari wenyewe ndio wanaimiliki na wao ndio waamuzi wa kuweka
habari katika mitandao hiyo na waliitaka jamii kuachana na habari kuwa
habari siyo lazima ikawa kwenye gazeti, redio na televisheni.
Mwisho
No comments:
Post a Comment