Na Gurian Adolf
Sumbawanga
WATU watano wamekufa maji katika ziwa Rukwa lililopo mkoani Rukwa wakati wakiwa katika shughuli za uvuvi katika ziwa hilo.
Tukio hilo lilitokea April 30 wakati watu hao wakiwa katika shughuli zao za uvuvi katika ziwa hilo.
Akitoa
taarifa ya tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Polycarp
Urio alisema kuwa watu hao walikuwa wakifanya shughuli za uvuvi katika
ziwa hilo.
Urio alisema
kuwa wavuvi walio kufa maji ni wakazi wa kijiji cha Ilanga, kata ya
Muze, tarafa ya Mtowisa, wilaya ya Sumbawanga, Mkoani humo.
Aliwataja
wavuvi hao kuwa ni Paschal Kipeza(30),Peter William(45), Edward
Emily(40),Frank Kadima(36) Pamoja na Saliboko Damasi(28) wote hao
wanasadikika kufa maji baada ya boti walilokuwa wakifanyia uvuvi
kuzama.
Kaimu kamanda
huyo alisema kuwa sababu ya kuzama kwa mtumbwi huo kulitokana na Mtumbwi
huo kukumbwa na dhoruba ya upepo mkali na kusababisha kuzama.
Aidha
katika tukio hilo mvuvi mmoja aitwaye Florence Mpomwa(27)alinusurika
kufa baada ya kujiokoa kwa kutumia dumu la maji ambalo lilimsaidia
kuelea hadi kufika nchi kavu na kuokolewa na wavuvi wengine.
Hata hivyo alisema kuwa miili ya marehemu hao imekabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi.
Kaimu
Kamanda Urio alitoa wito kwa wananchi hasa wavuvi kuwa makini
wanapokuwa katika shughuli zao za uvivu hasa katika kipindi hiki cha
masika.
Aliongeza kwa
kutoa ushauri kwa wavuvi wote waachane na uvivu haramu kwani ni kinyume
cha sheria za nchi na endapo watabainika hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
Mwisho
No comments:
Post a Comment