Saturday, 21 December 2013
MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEMPACHIKA MIMBA MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA.
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuachia huru Gelald Gabriel (18) mkazi wa mtaa wa Kawajense aliyekuwa mshitakiwa wa kesi ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya Msingi Msakila (15) kwa madai ya kutenda kosa hilo akiwa na umri mdogo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Chiganga aliieleza mahakama kuwa wakati mshitakiwa anatenda kosa hilo desemba 17 mwaka jana alikuwa na umri wa miaka 17 na kutokana na sheria namba 119 inakataza kumuhukumu kifungo cha kwenda jela mtu ambaye hajatimiza umri wa miaka 18.
Hakimu Chiganga alisema kuwa Mshitakiwa kutenda kosa hilo la kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi huyo nyakati za saa tatu asubuhi nyumbani kwa mjomba wake ambapo wazazi wa msichana walikuwa wamepanga kwenye nyumba hiyo.
Mshitakiwa alidaiwa kumbaka msichana huyo baada ya kuona kuwa watu wote waliokuwa wanaishi kwenye nyumba hiyo wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao za kila siku.
Awali kabla ya kusoma hukumu hakimu hiyo, Hakimu Chiganga alimpa mshitakiwa nafasi ya kujitetea ambapo aliiomba mahakama imwachie huru kutokana na umri wake kuwa mdogo wakati akitenda kosa hilo, pia alidai kuwa msichana huyo alikuwa akiishi na mjomba wake ambaye alikuwa hana mke hivyo hata huo ujauzito msichana huyo anaweza akawa alipewa na huyo mjomba wake waliokuwa wakiishi naye.
Mwendesha mashitaka mkaguzi wa Polisi, Ally Mbwijo, baada ya utetezi huo aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa kwani umri sio kigezo cha kumfanya mshitakiwa atende kosa hilo kwa makusudi.
Hata hivyo Hakimu huyo akisoma hukumu hiyo kwa kueleza hivyo mshitakiwa Gelald amenufaika na sheria hiyo hivyo mahakama inamwachia huru na asirudie tena kutenda kosa hilo baada ya kuachiwa huru.
CARITAS NA MAENDELEO SUMBAWANGA YATOA MSAADA
MFUKO wa Calitasi na maendeleo wa jimbo katoliki
Sumbawanga lililopo mkoani Rukwa umetoa
msaada wa mabati 40
yenye thamani ya shilingi 500,000 kwa wahanga wa mvua kubwa ya mawe iliyonyesha katika kijiji cha Kasense kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya
Sumbawanga mkoani humo.
Akikabidhi msaada huo kwa serikali ya kijiji mkurugenzi wa mfuko huo Padre Demetrius
Kazonde alisema kuwa lengo la msaada huo ni kuwasaidia baadhi ya watu
ambao nyumba zao ziliezuliwa kabisa paa
ili wazikarabati upesi na warejee katika nyumba zao waondokane na usumbufu
wanaoupata.
Alisema kuwa kutokana na kuwa tukio lenye ni dharula mfuko
huo ulitafuta fedha hizo kidogo na kuanza kutoa huku akiwaomba watu wenye
mapenzi mema wajitolee ili kuwasaidia watanzania wenzao wali katika wakati
mgumu kuliko kusubilia serikali ndiyo iwasaidie watu hao.
Katika msaada huo padre huyo alikabidhi pia fedha taslimu
kiasi cha shilingi 300,000 ambazo alisema alitumwa na askofu wa Kanisa Katoliki
jimbo la Sumbawanga Damian Kyaruzi
ambapo alisema askofu huyo alitoa fedha hizo ili ziwasaidie wahanga hao
katika wakati huo mgumu walio nao.
Naye Ofisa mtendaji
wa kijiji hicho Joseph Nandi alisema kuwa wameupokea msaada huo kwa mikono
miwili hasa katika kipindi hiki ambacho wakazi wa kijiji hicho wapo katika
wakati mgumu kutokana na wengine kubomoka kwa nyumba zao na hivyo hawana kwa
kuishi.
Alisema kuwa wananchi hao wamekuwa wakisaidiana kwani baadhi
waliwachukua watu ambao nyumba zao zimeharibika na kuwapa hifadhi hali
iliyosababisha kugawana chakula kidogo walicho nacho na hivyo kuhitaji msaada
mkubwa ili waweze kuishi katika mazingira bora zaidi.
Akishukuru wa niaba ya watu ambao nyumba zao zilibomoka
kufuatia mvua hiyo Peter Mwanisawa alisema kuwa
msaada huo umetolewa katika wakati muafaka kwani wengi wa watu ambao nyumba zao
ziliboka wanahitaji msaada wa vifaa vya ujenzi kwani ukarabati wa nyumba hizo
unahitaji fedha nyingi na bahati mbaya hawana fedha za kuweka kufanya ukarabati
huo.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kasense wakiangalia msaada wa mabati uliotolewa na mfuko wa Caritas na maendeleo jimbo Katoliki Sumbawanga na kiasi cha fedha taslimu shilingi 300,000
zilitolewa na Askofu Damian Kyaruzi wa kanisa Katoliki jimbo la Sumbawanga kwa wahanga hao msaada wote huo ulikabidhiwa kwa serikali ya kijiji.
zilitolewa na Askofu Damian Kyaruzi wa kanisa Katoliki jimbo la Sumbawanga kwa wahanga hao msaada wote huo ulikabidhiwa kwa serikali ya kijiji.
JELA MIAKA 60 KWA UNYANG'ANYI WA SILAHA.
WAKAZI wawili wa kijiji cha Kakese John
Mwakalebene (24) na Kamili Lugoye (30) wametiwa
hatiani na kuhukumiwa na makakama ya wilaya ya Mpanda mkoani
Katavi kutumikia kifungo cha miaka 60 jela kwa pamoja
baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda baada ya mahakama kutokuwa na shaka na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na pande mbili za mashitaka na utetezi ambapo kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka 30 jela.
Washitakiwa hao walidaiwa kutenda kosa hilo la unyang’anyi hapo Julai 7 mwaka huu saa mbili na nusu usiku kijijini hapo ambapo walimshambulia kwa mapanga Tija Sailasi na kisha kumpora fedha tasilimu Tsh 430,000.
Katika tukio hilo pia walipola simu mbili zenye thamani ya shilingi laki moja vitenge vya wax bunda za sigara aina ya SM na vocha na kufanya vitu thamani ya vitu na pesa walivyopola kuwa na jumla ya Tsh 760,000
Akisoma hukumu hiyo Hakimu, Chiganga Ntengwa baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi mahakama yake imewaona washitakiwa wamepatikana na kosa kwa mujibu wa sheria namba 287(A) ya sura ya 16 ya marekebisho ya mwaka 2009
Washitakiwa wakijitetea waliiomba mahakama hiyo iwapunguzie adhabu kutokana na umri wao kuwa mdogo na wameoa hivi karibuni na wazazi wao wanawategemea lakini baada ya maombi hayo, mwendesha mashitaka Mkaguzi msaidizi wa Polisi, Ally Mbwijo alipinga vikali na kuiomba mahakama itoe adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo kwani vitendo hivyo vimeshamiri sana Mkoa wa Katavi.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda baada ya mahakama kutokuwa na shaka na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na pande mbili za mashitaka na utetezi ambapo kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka 30 jela.
Washitakiwa hao walidaiwa kutenda kosa hilo la unyang’anyi hapo Julai 7 mwaka huu saa mbili na nusu usiku kijijini hapo ambapo walimshambulia kwa mapanga Tija Sailasi na kisha kumpora fedha tasilimu Tsh 430,000.
Katika tukio hilo pia walipola simu mbili zenye thamani ya shilingi laki moja vitenge vya wax bunda za sigara aina ya SM na vocha na kufanya vitu thamani ya vitu na pesa walivyopola kuwa na jumla ya Tsh 760,000
Akisoma hukumu hiyo Hakimu, Chiganga Ntengwa baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi mahakama yake imewaona washitakiwa wamepatikana na kosa kwa mujibu wa sheria namba 287(A) ya sura ya 16 ya marekebisho ya mwaka 2009
Washitakiwa wakijitetea waliiomba mahakama hiyo iwapunguzie adhabu kutokana na umri wao kuwa mdogo na wameoa hivi karibuni na wazazi wao wanawategemea lakini baada ya maombi hayo, mwendesha mashitaka Mkaguzi msaidizi wa Polisi, Ally Mbwijo alipinga vikali na kuiomba mahakama itoe adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo kwani vitendo hivyo vimeshamiri sana Mkoa wa Katavi.
Friday, 20 December 2013
MVUA YALETA MADHARA KIJIJI CHA KASENSE
Baadhi ya Nyumba zilizo bomoka na kuezuliwa paa katika kijiji cha Kasense kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyonyesha kwa muda wa masaa mawili.
KING'AMUZI CHA TING CHAZINDULIWA RUKWA.
KAMPUNI ya AGAPE
televisheni imezindua na kuanza
kuuza kisimbusi chake cha aina ya TING mkoani Rukwa ili kutoa fursa kwa wakazi
wa mkoa huo kuanza kutumia teknolojia ya digitali ambapo wataweza kuona channel
nyingi tofauti na kutumia teknolojia ya Analojia ambayo haitoi fursa ya kupata chaneli nyingi
kama ilivyo kwenye Digitali.
Akizindua kisimbusi
hicho kwa niaba ya mkuu wa mkoa
huo ,makamu mwenyekiti wa
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
Emmanuel Malisawa alisema kuwa hii ni fursa kwa wakazi wa mkoa
huo kuingia katika mfumo wa digital mapema zaidi kuliko kusubiri mpaka serikali
itakapo zima mitambo ya Analojia ndipo waanze kutumia visimbusi vitakavyo
wawezesha kupata matangazo ya televisheni.
Alisema kuwa
mabadiliko hayo ya kiteknolojia ni fursa nzuri kwa wakazi wa mkoa huo
ambao ulikuwa haupati vyombo vya habari vingi katika mfumo wa analojia lakini
kwa mfumo huu mpya wakazi wake watakuwa na uamuzi wa kuchagua kuangalia
televisheni wanayotaka.
Naibu meya alisema kuwa kutokana na madiliko hayo wakazi wa
Rukwa wanafursa ya kujua mambo mengi ikiwemo na masuala ya kibiashara ambapo
kupitia ongezeko la vyombo vya habari wataweza pia kujua bei ya vitu mbalimbali
ikiwemo soko la zao la mahindi ambalo imekuwa ni tatizo kwa wakulima waliopo
mkoani humo.
Kwaupande wake mkurugenzi wa
Kampuni ya Agape Televisheni Vennon
Fernandos wanaomiliki kisimbusi cha TING
alisema kuwa wameamua kuja mkoani Rukwa kwa nia mbili kwanza ikiwa ni
kutoa fursa kwa wakazi wa mkoa huo kuingia katika mfumo wa digitali mapema
zaidi ambapo watapata nafasi ya kusikia na kujifunza mambo ya watu wengine
sambamba na wao kutangaza yakwao.
Alisema kuwa sababu nyingine ni kuhubiri neno la mungu
kupitia chaneli za kidini zinazopatika katika kisimbusi hicho ambapo kinaongeza
wigo wa kusikia neno la Mungu hata ukiwa nyumbani kwako injili itakufikia hapo
ulipo.
POKEA KING'AMUZI HIKI UKATUMIE NYUMBANI KWAKO.
Mkurugenzi wa ATN Televisheni Nabii na Askofu Veron Fernandos akimkabidhi kisimbusi cha TING mmoja wa wachungaji mkoani Rukwa wakati akizindua kisimbuzi hicho ambacho kinanasa matangazo ya Digitali mkoani Rukwa.
Thursday, 19 December 2013
VIBAKA WATEMBEZA KIPIGO KATIKA BAA MBALIMBALI SUMBAWANGA
BAADHI ya wakazi wa mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa
wamelelamikia kuwepo kwa kundi la vibaka
wanaoendesha vitendo vya uvamizi katika maeneo tofauti ya kuuzia vilevi na
kisha kuwatembezea kipigo watu wanaowakuta katika maeneo hayo na kuwapora vitu mbalimbali ikiwemo fedha
taslimu.
Kikundi hicho kimekuwa kikivamia katika baa zilizopo
uchochoroni na kisha kuwalazimisha wateja wanao wakuta kutoa simu na fedha
walizonazo na kisha kumvamia muhudumu na kuchukua fedha zote za mauzo na
kuondoka nazo kuelekea kusikojulikana.
Peter Joachim ni
mmoja wa watu walivamiwa katika baa
ijulikanayo kwa jina la Lusaka Pub iliyopo mjini humo alisema kuwa
wakiwa wanaendelea na burudan zao majira wa saa 5;15 za usiku lilitokea kundi
la watu sita wakiwa na nondo na mapanga na kuingia ghafla ndani ya baa hiyo na
kuwataka walale chini na kwa yeyote atakaye kataa kutii amri hiyo atauawa.
Alisema kutokana na silaha hizo walizokuwa nazo watu wote
walilala chini na kisha vibaka hao waliwataka watoe fedha zote walizokuwa nazo
pamoja na simu na kisha kuanza kuwakagua na waliporidhika kuwa hawanakitu
waliondoka zao.
Katika tukio jingine lililotokea katika eneo la Wajanja Pub
kundi la watu waliokuwa na mapanga, marungu na nondo walivamia katika baa hiyo
ambapo walimkuta mtunza hazina wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Rukwa na kisha kumpora fedha zaidi ya shilingi
200,000 na kuondoka nazo.
Mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Lingatsova
alivamiwa akiwa mlangoni kwake na kundi la watu wasiojulikana na kisha kumpiga nondo katika maeneo
mbalimbali ya mwili wake na kisha kumpora fedha taslimu kiasi cha shilingi
250,000 pamoja na simu aina ya Sumsung Galaxy na kisha kuondoka nazo.
Baada ya kumpora
mtunza hazina huyo vibaka hayo
walivamia katika nyumba ya mwanamke
mmoja ili nako wafanye uporaji huo lakini mwanamke huyo aliwaona na kupiga
kelele ambapo vibaka hao walitimua mbio
na kuelekea kusikojulikana.
Subscribe to:
Posts (Atom)