Saturday, 21 December 2013
MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEMPACHIKA MIMBA MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA.
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuachia huru Gelald Gabriel (18) mkazi wa mtaa wa Kawajense aliyekuwa mshitakiwa wa kesi ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya Msingi Msakila (15) kwa madai ya kutenda kosa hilo akiwa na umri mdogo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Chiganga aliieleza mahakama kuwa wakati mshitakiwa anatenda kosa hilo desemba 17 mwaka jana alikuwa na umri wa miaka 17 na kutokana na sheria namba 119 inakataza kumuhukumu kifungo cha kwenda jela mtu ambaye hajatimiza umri wa miaka 18.
Hakimu Chiganga alisema kuwa Mshitakiwa kutenda kosa hilo la kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi huyo nyakati za saa tatu asubuhi nyumbani kwa mjomba wake ambapo wazazi wa msichana walikuwa wamepanga kwenye nyumba hiyo.
Mshitakiwa alidaiwa kumbaka msichana huyo baada ya kuona kuwa watu wote waliokuwa wanaishi kwenye nyumba hiyo wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao za kila siku.
Awali kabla ya kusoma hukumu hakimu hiyo, Hakimu Chiganga alimpa mshitakiwa nafasi ya kujitetea ambapo aliiomba mahakama imwachie huru kutokana na umri wake kuwa mdogo wakati akitenda kosa hilo, pia alidai kuwa msichana huyo alikuwa akiishi na mjomba wake ambaye alikuwa hana mke hivyo hata huo ujauzito msichana huyo anaweza akawa alipewa na huyo mjomba wake waliokuwa wakiishi naye.
Mwendesha mashitaka mkaguzi wa Polisi, Ally Mbwijo, baada ya utetezi huo aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa kwani umri sio kigezo cha kumfanya mshitakiwa atende kosa hilo kwa makusudi.
Hata hivyo Hakimu huyo akisoma hukumu hiyo kwa kueleza hivyo mshitakiwa Gelald amenufaika na sheria hiyo hivyo mahakama inamwachia huru na asirudie tena kutenda kosa hilo baada ya kuachiwa huru.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment