BAADHI ya wakazi wa mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa
wamelelamikia kuwepo kwa kundi la vibaka
wanaoendesha vitendo vya uvamizi katika maeneo tofauti ya kuuzia vilevi na
kisha kuwatembezea kipigo watu wanaowakuta katika maeneo hayo na kuwapora vitu mbalimbali ikiwemo fedha
taslimu.
Kikundi hicho kimekuwa kikivamia katika baa zilizopo
uchochoroni na kisha kuwalazimisha wateja wanao wakuta kutoa simu na fedha
walizonazo na kisha kumvamia muhudumu na kuchukua fedha zote za mauzo na
kuondoka nazo kuelekea kusikojulikana.
Peter Joachim ni
mmoja wa watu walivamiwa katika baa
ijulikanayo kwa jina la Lusaka Pub iliyopo mjini humo alisema kuwa
wakiwa wanaendelea na burudan zao majira wa saa 5;15 za usiku lilitokea kundi
la watu sita wakiwa na nondo na mapanga na kuingia ghafla ndani ya baa hiyo na
kuwataka walale chini na kwa yeyote atakaye kataa kutii amri hiyo atauawa.
Alisema kutokana na silaha hizo walizokuwa nazo watu wote
walilala chini na kisha vibaka hao waliwataka watoe fedha zote walizokuwa nazo
pamoja na simu na kisha kuanza kuwakagua na waliporidhika kuwa hawanakitu
waliondoka zao.
Katika tukio jingine lililotokea katika eneo la Wajanja Pub
kundi la watu waliokuwa na mapanga, marungu na nondo walivamia katika baa hiyo
ambapo walimkuta mtunza hazina wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Rukwa na kisha kumpora fedha zaidi ya shilingi
200,000 na kuondoka nazo.
Mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Lingatsova
alivamiwa akiwa mlangoni kwake na kundi la watu wasiojulikana na kisha kumpiga nondo katika maeneo
mbalimbali ya mwili wake na kisha kumpora fedha taslimu kiasi cha shilingi
250,000 pamoja na simu aina ya Sumsung Galaxy na kisha kuondoka nazo.
Baada ya kumpora
mtunza hazina huyo vibaka hayo
walivamia katika nyumba ya mwanamke
mmoja ili nako wafanye uporaji huo lakini mwanamke huyo aliwaona na kupiga
kelele ambapo vibaka hao walitimua mbio
na kuelekea kusikojulikana.
No comments:
Post a Comment