Sumbawanga
KIJANA ambaye hakuweza kufahamika jina lake wala anapoishi amenusurika kifo majira ya asubuhi katika maeneo ya benki ya NMB mjini Sumbawanga mkoani Rukwa,baada ya baiskeli aliyokuwa akiendesha kugongwa na gari.
Tukio
hilo lilitokea ghafla Mara baada ya gari kuigonga baiskeli hiyo na
kusababisha taili la mbele kupinda mara baada ya gari hilo kuigonga
baiskeli hiyo.
Mwandishi
wa habari hii alishuhudia tukio hilo ambapo anasimulia kuwa gari hilo
lilipoteza uelekeo na kwenda kuigonga baiskeli hiyo.
Pamoja
na kuharibika baiskeli hiyo lakini mtu ambaye jina lake halikufahamika
Mara moja aliyekuwa anaendesha baiskeli hiyo alinusurika.
Baada ya tukio hilo polisi wa usalama barabarani walifika muda mfupi na kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
Hata
hivyo taratibu za kisheria zinaendelea kufuatia tukio hilo kwani askali
hao wa usalama barabarani waliwachukua watu waliohusika na tukio hilo
na kuelekea nao katika kituo cha polisi kilichopo mjini Sumbawanga.
Mwisho
No comments:
Post a Comment