MFUKO wa Calitasi na maendeleo wa jimbo katoliki
Sumbawanga lililopo mkoani Rukwa umetoa
msaada wa mabati 40
yenye thamani ya shilingi 500,000 kwa wahanga wa mvua kubwa ya mawe iliyonyesha katika kijiji cha Kasense kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya
Sumbawanga mkoani humo.
Akikabidhi msaada huo kwa serikali ya kijiji mkurugenzi wa mfuko huo Padre Demetrius
Kazonde alisema kuwa lengo la msaada huo ni kuwasaidia baadhi ya watu
ambao nyumba zao ziliezuliwa kabisa paa
ili wazikarabati upesi na warejee katika nyumba zao waondokane na usumbufu
wanaoupata.
Alisema kuwa kutokana na kuwa tukio lenye ni dharula mfuko
huo ulitafuta fedha hizo kidogo na kuanza kutoa huku akiwaomba watu wenye
mapenzi mema wajitolee ili kuwasaidia watanzania wenzao wali katika wakati
mgumu kuliko kusubilia serikali ndiyo iwasaidie watu hao.
Katika msaada huo padre huyo alikabidhi pia fedha taslimu
kiasi cha shilingi 300,000 ambazo alisema alitumwa na askofu wa Kanisa Katoliki
jimbo la Sumbawanga Damian Kyaruzi
ambapo alisema askofu huyo alitoa fedha hizo ili ziwasaidie wahanga hao
katika wakati huo mgumu walio nao.
Naye Ofisa mtendaji
wa kijiji hicho Joseph Nandi alisema kuwa wameupokea msaada huo kwa mikono
miwili hasa katika kipindi hiki ambacho wakazi wa kijiji hicho wapo katika
wakati mgumu kutokana na wengine kubomoka kwa nyumba zao na hivyo hawana kwa
kuishi.
Alisema kuwa wananchi hao wamekuwa wakisaidiana kwani baadhi
waliwachukua watu ambao nyumba zao zimeharibika na kuwapa hifadhi hali
iliyosababisha kugawana chakula kidogo walicho nacho na hivyo kuhitaji msaada
mkubwa ili waweze kuishi katika mazingira bora zaidi.
Akishukuru wa niaba ya watu ambao nyumba zao zilibomoka
kufuatia mvua hiyo Peter Mwanisawa alisema kuwa
msaada huo umetolewa katika wakati muafaka kwani wengi wa watu ambao nyumba zao
ziliboka wanahitaji msaada wa vifaa vya ujenzi kwani ukarabati wa nyumba hizo
unahitaji fedha nyingi na bahati mbaya hawana fedha za kuweka kufanya ukarabati
huo.
No comments:
Post a Comment